22.5 C
Dar es Salaam
Friday, June 21, 2024

Contact us: [email protected]

Nameless aingilia ugomvi wa Octopizzo na Wahu

NamelessNAIROBI, KENYA

MSANII wa muziki nchini Kenya, David Mathenge ‘Nameless’, ameingilia kati mgogoro wa mke wake, Wahu na msanii mwenzake, Octopizzo, baada ya wawili hao kutupiana maneno kwenye mitandao ya kijamii.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, Octopizzo alifanikiwa kupata Bingwa Awards nchini humo, lakini baada ya kupewa aliandika kwenye mtandao wake wa Twitter kwamba kutokana na ubora wake hakustahili kupata tuzo hiyo ila aliyestahili ni Wahu.

Ujumbe huo ulikuwa unamaanisha kwamba, Wahu ana uwezo mdogo wa kufanya muziki tofauti na Octopizzo, hata hivyo alisababisha malumbano ambayo Nameless ameamua kuingilia kati kwa kumtetea mke wake.

“Tuheshimiane kaka! Umepata tuzo alafu unadai kwamba siyo yako na kwa dharau unampa Wahu? Unatakiwa kujiheshimu tambua ipo siku utakuja kutafuta tuzo katika maisha yako uliyopata itakulinda na kukupa heshima. Jiheshimu uheshimiwe acha kufuatilia maisha ya Wahu,” aliandika Nameless.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles