Wizkid adaiwa kuiba wimbo wa ‘Ojuelegba’

0
1220

wizkidLAGOS, NIGERIA

MKALI wa muziki nchini Nigeria, Ayodeji Balogun ‘Wizkid’, amedaiwa kuiba wimbo unaofanya vizuri kwa sasa ujulikanao kwa jina la ‘Ojuelegba’.

Nyota wa hip hop nchini humo, Ahmedu Augustine ‘Blackface’, amedai kwamba Wizkid amekuwa na tabia ya kuiba nyimbo zake lakini amekuwa kimya kwa muda mrefu ila sasa ameamua kuvunja ukimya wake.

“Nilikuwa kimya kwa siku nyingi, lakini kwa sasa nimeona bora niweke wazi kwa kuwa kwenye wimbo wangu mpya wa ‘Killa’ midundo yake ni kama wimbo huo wa Wizkid, kitu ambacho sikipendi.

“Hata hivyo, ukiusikiliza wimbo wangu wa ‘Dancehall’ ambao niliuachia mwaka 2010 unafanana na huu wa Ojuelegba, lakini kikubwa ni kuisikiliza albamu hiyo kisha utagundua ukweli kuhusu hili. Najua hata yeye mwenyewe anajua hilo,” aliandika Blackface kupitia mtandao wa Instagram.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here