25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

NAMBA  YA JEZI  INAVYOAKISI UBORA WA MCHEZAJI

ADAM MKWEPU NA MITANDAO


USHAHIDI wa  namba  ya jezi  inavyoweza akisi ubora wa mchezaji ulionekana  dhahili wiki iliyopita kwa  mwanasoka mmoja aitwaye Yado Mambo ambaye hakuva jezi namba 5.

Wakati wa mechi ya ligi kati ya Leyton Orient na Ebbsfleet United, ambayo mlinzi wake wa  kati Mambo (26) alidaiwa kushindwa kufanya vizuri kwa sababu benchi la ufundi halikumpa jezi yenye tarakimu ya tano,  kama heshima ya namba 5 ilivyokuwa kwa mwanamuziki maarufu wa Kijeruman, Lou Bega aliyeachia kibao chake cha ‘Mambo namba tano ’ mwaka 1999.

“Fikiria kusaini mchezaji aitwaye Mambo na hakumpa jezi namba tano,  alimtuhumia mtumiaji mmoja wa ukurasa wa Twitter akipiga picha jezi namba 18 aliyovaa nyota huyo, wakati wa mchezo. “Tuko chini ya ubora Ebbsfleet United.” Alimaliza shabiki huyo.

Akizungumza na Radio Kent  ya Uingereza, Mambo alionyesha kwamba alikuwa ameomba jezi  yenye namba 5 kabla ya msimu kuanza, lakini  ombi hilo lilionekana kupigwa chini na Meneja wa klabu hiyo, Daryl McMahon.  “Nilimwambia mwakilishi wangu jambo hilo, lakini sidhani alianiamini hadi lililopozungumzwa na mashabiki katika mitandao ya kijamii wiki hii (iliyopita).

“Labda sasa watalichukulia kwa uzito zaidi na kubadilisha namba yangu msimu ujao. Mambo namba tano  ilikuwa moja ya nyimbo zangu zipokuwa zikivuma katika umri huo. Kwenye shule watoto wengi walitumia kuimba.”

Klabu ya Ebbsfleet  wanatakiwa kukubaliana  na  jambo hili kwa kuwa na jezi hiyo kwa ajili ya kufanya biashara, mashabiki wa klabu hiyo wameonekana kuwa tayari kununua kwa wingi jezi hiyo.

Tunaweza kuwa na matumaini ya klabu ya Tottenham Hotspur kuhusu namba nne ya Luke Amos na mwenzake  Harry Winks, tangu  walipofungua majadiliano.

Katika mtazamo tofauti, namba za jezi haina maana zaidi ya kitambulisho, lakini kuna dhana zaidi hayo. Baadhi ni utambulisho ikienda sambamba na utamaduni unaohusishwa na ujuzi na ubunifu ndani ya uwanja.

Si kila mchezaji wa zamani alikuwa akipenda kuvaa namba kumi. Neno moja kutoka Uwanja wa Emirates linasema kwa  kuzingatia  jezi fulani ya Arsenal iliyovaliwa kwenye mabega ya Jack Wilshere.

Katika historia yake, Harry Redknapp alibainisha kuwa mwaka wa 1996,  West Ham mpya ilimsajili Paulo Futre kutoka Arsenal, katika ufunguzi wa msimu na kupewa jezi namba 16.

“Futra anavaa  namba 10 si namba 16,” nyota huyo alimweleza kocha wake aliyekuwa amesimama na kuongeza kwamba: “Eusebio namba 10, Maradona namba 10, Pelé namba  10, Futra  namba 10 si 16. Kwa msaada wa wanasheria wake na ahadi ya kubadilishiwa jezi hiyo iliyokuwa ikivaliwa na mkongwe John Moncur, Futre hatimaye alipata kile alichokihitaji.

Wachezaji wengine hawajawahi kuwa katika kiwango kikubwa sana, badala ya kuchagua jezi ambazo walitumia wachezaji mahiri.Wakati Roberto Baggio akijiunga na Inter Milan mwaka 1998 na alisisitiza kuhusu kuchukua jezi ya Ronaldo de Lima ya namba 10, mshambuliaji huyo wa Brazili alionywa kitendo hicho na Iván Zamorano. Maamuzi ya dhati ni kitu muhimu, mshambuliaji raia wa Chile ambaye alikuwa akicheza Inter Milan uamuzi huo wanauita “Bam Bam”, namba aliyochagua wakati huo ilikuwa  1 + 8. Ikiwa na maana 9.

Wachache walianza maandamano ya Ronaldo wa Brazili kwa kumpinga yule Roanldo wa Kireno, wakidai kwamba kuna Ronaldo mmoja tu chini ya jua.

Lakini baada ya kunyakuwa tuzo ya mchezaji bora mara nne kila kitu kimebadilika, kwa sasa ametengeneza nembo yake mwenyewe CR7. Kwa watu wengi wa umri fulani namba saba itaendelea kuwa jina kubwa la mpambanaji wa vita kama ilivyokuwa kwa  Mad Jack, mjumbe wa kikundi cha ‘The Life And Times’ chini ya  Grizzly Adams.

Lakini katika mazingira ya mchezo wa soka inakumbusha juhudi za nguli wa mchezo huo kama vile, Manuel Francisco, ‘Garrincha’, Luis Figo, Eric Cantona, David Beckham, George Best na Kenny Dalglish.

Hata katika mchezo wa mpira wa meza imani hiyo inaonekana kwa mfano sehemu moja ya Seinfeld ilizingatia mpango wa nguli wa mchezo huo  George Costanza kumpa mwanawe wa kwanza  jina la ‘Seven’ kuthamini kile kilichofanywa na mkali  wa  New York Yankees,  Mickey Mantle aliyekuwa akivaa namba hiyo.

Aliyekuwa nyota wa Liverpool Andy Carroll pamoja na mchumba wake Billi Mucklow, hivi karibuni walimpa mtoto wao wa pili jina la namba anayovaa West Ham kwa sasa ‘Wolf Nine’.

Aliyekuwa kipa wa zamani wa  timu ya taifa Italia Gianluigi Buffon aliamua kuvaa jezi namba 88 akiwa katika timu yao  ikiwakasirisha watu wa Kiyahudi wa Italia, ambao waliiona kama ishara ya Nazi (H ni  ya nane katika orodha ya  alfabeti, hivyo 88 sawa na HH, au Heil Hitler).

Kipa huyo, aliyekuwa amepoteza nafasi yake katika timu ya taifa ya Italia kwa Francesco Toldo, alitoa maana ya siri na alisisitiza kwanini alichagua namba hiyo kwa kuwa ilikuwa ikiwakilisha wanawake wawili.

“Nimechagua 88 kwa sababu inanikumbusha mipira minne na Italia sisi sote tunajua nini maana ya kuwa na mipira minne, nguvu na uamuzi,” anasema na kuongeza “Na msimu huu nitakuwa na mipira hiyo ili niweze kurudi mahali pangu katika timu ya Italia.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles