31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

ADHABU ALIYOPEWA CIOABA HAITOSHI

Na ZAINAB IDDY


JUMATANO iliyopita Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara ilitoa adhabu ya kumfungia mechi tatu pamoja kutakiwa kulipa faini ya Shilingi 500,000, kocha wa Azam FC Mromania, Aristica Cioaba.

Adhabu hiyo imetolewa kwa Cioaba, kutokana na kukutwa na hatia ya kuwa bughudhi marefa kwenye mechi ya timu yake dhidi ya Ruvu Shooting, iliyochezwa Uwanja wa Chamanzi jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huo uliomalizika kwa Azam FC kushinda 1-0, bao lililopatikana kwenye dakika za nyongeza kupitia kwa mchezaji wao Yahaya Zayd.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura alipokuwa kizungumza na waandishi wa habari, alidai kuwa katika mchezo huo, Cioaba aliwafuata waamuzi kulalamikia kwa kurusha mikono akionyesha kutoridhika na maamuzi yao kwenye mechi namba 69, hivyo kuonekana akiwaghubudhi waamuzi  ikiwa ni kinyume cha sheria za soka kwa kuzingatia Kanuni ya 40(1) ya ligi kuhusu udhibiti wa makocha kwa waamuzi.

Pongezi kwa TFF kwa kuona na kulitolea mamauzi jambo lililokiuka kinyume na kanuni za ligi, lililofanywa na Cioaba ingawa Kiroho safi inaona adhabu aliyopewa haitoshi wala kukidhi ukubwa wa kosa alilofanya.

Inafahamika kitendo kilichofanywa na kocha wa Azam FC si kigeni kwenye mechi zinazosimamiwa na bodi ya ligi na imeshatolewa adhabu kama hiyo, lakini bado makocha wanaonekana kutojali na kuendelea na kile wanachoona ni sahihi.

Si mara moja tumeshuhudia makocha wanaofundisha ligi kuu na zile Daraja la Kwanza wakifungiwa mfano mzuri, Hemed Morocco alipokuwa akiifundisha Stand United, Hans van de Pluijm alipokuwa Yanga na wengine wengi, lakini imekuwa vigumu kutoacha kuwaghubudhi wamuzi wanapokuwa wakitimiza majukumu yao.

Ni kweli waamuzi nao ni binadamu,wanamakosa yao wanapokuwa kazini, lakini kwanini isisubiriwe mpira ukaisha kisha kocha akayafikisha wa viongozi wake wa juu wenye mamalaka ya kutoa malalamiko yao katika bodi ya ligi, ambayo inakazi kubwa ya kurejea kuangalia mpira na kujirizisha na zile ripoti zinazowafikia kisha kuzitolea maamuzi.

Lakini kitendo cha kutoa adhabu ya kukosa mechi tatu pamoja na faini ya kiasi hicho cha fedha ni jambo lisalokuwa na mashiko, wala kumfanya kocha kutorejea kosa lilolifanya mwenzake kwa kuwa anauhakika aruhusiwi kukaa kwenye benchi tu siku ya mechi, lakini majukumu yake anatimiza kama kawaida.

Ni wakati sasa kwa TFF kuongeza ukubwa wa adhabu ikiwemo hata kutompa nafasi ya kuambatana na timu kwa zaidi ya michezo 10, ambayo ni sawa na nusu msimu hii itakuwa suluhisho lakini kwa hii iliyotolewa kwa Cioaba haitoshi na haiwezi kuwa funzo, litakalozuia makocha wenye tabia hizi kuwaacha wamuzi wafanye kazi kwa uhuru.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles