25.3 C
Dar es Salaam
Thursday, December 2, 2021

Nadal atolewa robo fainali ya ATP

Britain Queens Tennis ChampionshipRIO DE JANEIRO, BRAZIL

NYOTA wa mchezo wa tenisi, Rafael Nadal, juzi alishindwa kutinga katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya ATP baada ya kupoteza mchezo wake dhidi ya Pablo Cuevas kwenye mashindano ya wazi ya Rio.

Bingwa huyo mara 14 wa Grand Slam, alianza kwa kuongoza kwa alama mbili katika seti mbili za mwanzo, lakini baadaye alianza kupoteza mchezo kwa kufungwa jumla ya seti 6-7 (6) 7-6 (3) 6-4.

Hata hivyo, pamoja na kupoteza mchezo huo, Nadal amesema amekubali kushindwa na atajaribu kulifanyia kazi na kubadili mwelekeo katika michuano mingine.

“Nakubali nimepoteza mchezo ambao ulikuwa muhimu sana kwangu, lakini sina jinsi, kikubwa ni kufanya maandalizi kwa ajili ya michuano mingine iliyopo mbele yangu kwa ajili ya kurudisha heshima yangu.

“Siwezi kuangalia kilichopita, kikubwa ni kuangalia nini nitafanya kwa kuwa bado nina uwezo wa kurudisha heshima yangu kwa mashabiki,” alisema Nadal.

Cuevas, ambaye anashikilia nafasi ya 45 ulimwenguni katika mchezo wa tenisi, atakutana na Guido Pella katika hatua ya fainali.

- Advertisement -
bestbettingafrica

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
167,640FollowersFollow
526,000SubscribersSubscribe
- Advertisement -
10Bet

Latest Articles