26.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 8, 2024

Contact us: [email protected]

Zidane: Ubingwa kwetu ni ndoto

zinedine-zidane-real-madridMADRID, HISPANIA

BAADA ya klabu ya soka ya Real Madrid juzi kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Malaga katika michuano ya Ligi Kuu nchini Hispania, kocha wa timu hiyo, Zinedine Zidane, ameweka wazi kwamba kuutwaa ubingwa msimu huu itakuwa ndoto kwao.

Kocha huyo anaamini kwamba wapinzani wao, Barcelona, wana nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa huo msimu huu kutokana na jinsi wanavyoshinda kwenye michezo yao na kwa sasa wanaongoza Ligi wakiwa na alama 63, wakifuatiwa na Atletico Madrid ambao wana alama 55, huku Madrid wakiwa na alama 54.

Katika mchezo wa juzi, Madrid ilishuka dimbani bila nyota wake, Karim Benzema na Gareth Bale na kumuanzisha Cristiano Ronaldo, ambaye ndiye aliyeifungia bao Madrid dakika ya 33.

Hata hivyo, dakika 2 baadaye Madrid wakapata penati ambayo Ronaldo akaipoteza baada ya kuokolewa na kipa wa Malaga, Carlos Kameni. Hii inakuwa penalti ya 7 kwa Ronaldo kukosa msimu huu, ikiwa ni idadi sawa na mpinzani wake, Lionel Messi.

“Itakuwa ngumu sana kuweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu, lakini haimaanishi baada ya kutoka sare na Malaga ndipo safari ya kupigania ubingwa kuwa imekatika, hapana, bado tunaendelea kupambana hadi mwisho.

“Kwa upande wa wapinzani wetu, Barcelona, wamekuwa katika kipindi kizuri na ndiyo maana wanashinda michezo yao, lakini na sisi tunaamini bado tuna kikosi kizuri, japokuwa kuna baadhi ya majeruhi kama vile Bale na Benzema, ila baada ya muda watakuwa uwanjani,” alisema Zidane.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles