29.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

NABII MWIGIRA SHINDA KESI YA KUZAA NA MKE WA MTU

Na KULWA MZEE-DAR ES SALAAM


NABII Josephat Mwingira ameibuka mshindi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam kutamka kwamba mdai ameshindwa kuthibitisha kama alizini na mkewe hadi kufanikiwa kupata mtoto wa kiume.

Hukumu hiyo ilitolewa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba kwa niaba ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mhini aliyesikiliza kesi hiyo.

Katika kesi hiyo ya madai, Dk. Willium Moris, alidai Nabii Mwingira alizini na kuzaa na mkewe, Dk. Philis Nyimbi, hivyo alipwe fidia ya Sh bilioni saba.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Simba alisema mahakama baada ya kupitia ushahidi, imeona mdai, Dk. Morris ameshindwa kuthibisha mahusiano ya mapenzi kati ya mkewe Dk. Nyimbi na Nabii Mwingira.

Pia mahakama hiyo imeona mdai kashindwa kuthibitisha kwamba mtoto aliyezaliwa alitokana na uzinzi na ni wa Nabii Mwingira.

“Mdai kashindwa kwa kiwango cha kesi za madai, hivyo mahakama inamtaka alipe gharama zote za kesi alizotumia Nabii Mwingira na Dk. Nyimbi,” alisema Hakimu Simba.

Akizungumza baada ya hukumu hiyo, wakili wa mdai, Respicius Ishengoma, alisema lazima wakate rufaa kutafuta haki.

“Lazima tukate rufaa, katika kesi kama hii ya mtoto, suluhisho pekee lilikuwa kupima DNA, lakini mahakama ilikataa na mdaiwa pia alikataa, hiyo ndiyo sababu kubwa ya rufaa yetu, apime DNA jibu linapatikana,” alisema Ishengoma.

Awali katika ushahidi kwenye kesi hiyo, Nabii Mwingira na Dk. Nyimbi wote walikana kuzaa mtoto huyo.

Pia Dk. Nyimbi akidai haujui mwili wa Nabii Mwingira na kwamba mtoto ni wake alizaa na Baraka ambaye ni marehemu.

Dk. Morris alidai Nabii Mwingira alizini na mkewe na kuzaa naye mtoto wa kiume ambaye wakati akifungua kesi hiyo alikuwa na umri wa miaka tisa.

Katika kuthibitisha hilo, Dk. Morris alileta shahidi mmoja mahakamani ambaye alielekeza ushahidi wake katika maelezo ya aliyekuwa mke wa Dk. Morris, Dk. Nyimbi aliyotoa Polisi Kibaha.

Shahidi huyo, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Evans Mwijage, alida Dk. Nyimbi alikwenda kwa Nabii Mwingira kufanyiwa maombi ili mumewe aliyekuwa Marekani arudi nchini, lakini badala ya kumfanyia maombi alizini naye hadi wakafanikiwa kupata mtoto wa kiume.

Alidai Dk. Nyimbi alitambulishwa kwa Nabii Mwingira, alipokewa na alimtambulisha kwa waumini wote kwamba ni ndugu yake, wakapeana namba za simu wakawa wanawasiliana.

“Dk Philis alieleza shida yake ni maombi ili mumewe arejee nchini, siku moja Nabii Mwingira akampigia simu akamwelekeza amfuate Millenium Tower Hotel akamfanyie maombi, alimjibu hapajui, akamwambia akodi teksi atafika, akifika aulize mapokezi ataelekezwa chumba alichokuwemo,” alidai shahidi huyo.

Mwijage aliendelea kudai kwamba Dk. Nyimbi alikwenda hotelini muda wa saa mbili usiku, ambako alimkuta Nabii Mwingira yuko sebuleni peke yake akadhani bado waumini wengine wataendelea kufika kwa maombi.

Alidai Nabii Mwingira alimwagizia soda ya Sprite huku yeye akinywa maji ya moto, walipomaliza kunywa alielekezwa na Nabii huyo aingie chumbani akapumzike.

“Anadai baada ya tendo hilo Nabii Mwingira aliondoka, Dk. Philis akabakia hadi asubuhi ndipo alipoamua kuondoka hotelini, hakupiga kelele wakati tendo likiendelea kwa sababu aliogopa aibu na hakutoa taarifa polisi, aliogopa kumvunjia heshima Nabii. Waliendelea kufanya hivyo na siku nyingine.

“Siku chache baadae alijiona hayuko sawa na alipofuatilia alikuwa tayari mjamzito, alimfahamisha Nabii akamwambia atoe ama azae, yeye aliamua kuzaa, wakati ulipofika alijifungua mtoto wa kiume,” alidai.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles