22.5 C
Dar es Salaam
Saturday, June 22, 2024

Contact us: [email protected]

Mzungu wa Twaha Kiduku kutua kesho

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

MPINZANI wa bondia wa ngumi za kulipwa nchini Twaha Kiduku, Lago Kiziria kutoka Taifa la Georgia anatarajia kuwasili kesho jijini Dar es Salaam kisha kuelekea mkoani Morogoro tayari kwa pambano la ngumi la raundi nane lililopewa jina la Mfalme mwenye Ufalme Wake litakalopigwa Aprili 22, 2023, Morogoro.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 18, 2023 jijini Dar es Salaam wakati mabondia watakaosindikiza pambano hilo wakipima afya, Mratibu wa Habari wa Peaktime Media waandaaji mchezo huo,Victor Denis, amesema kuwasili kwa Kiziria ni ishara kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 100.

“Pambani hili litakuwa la kihistoria kwani tofauti na Kiziria kuwasili, bondia, Loren Japhet ambaye ni Mtanzania anayeishi Ghana atatua nchini ambapo atazichapa na Juma Choki,” amesema Denis.

Mratibu huyo amesema siku hiyo kutakuwa na jumla ya mapambano nane yakihusisha mabondia kutoka mikoa tofauti nchini, huku moja likiwa la wanawake ambapo Sara Alex wa Arusha atapigana na Flora Machela wa Dar es Salaam.

Amewataka wakazi wa Morogoro na mikoa ya jirani kujitokeza kwa wingi kushudia burudani ya masumbwi ikiwamo kuona vipaji vipya vya ndondi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles