31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

MZOESHE MTOTO KUSOMA VITABU


NA AZIZA MASOUD

MTOTO anapozaliwa mzazi anakuwa na jukumu  la kumuwekea mazingira ya kujifunza mambo mbalimbali ili aweze kuwa na uelewa mpana katika baadhi ya vitu.

Mafunzo ya  mtoto yanayotolewa na mzazi si namna ya kuishi na watu tu na kuwaheshimu wengine, bali mtoto anapaswa kupata mambo mengine ya ziada ambayo yanaweza kumsaidia kujifunza vitu vingi ambavyo vitakuja kumuonyesha mwanga katika maisha yake ya baadaye.

Yapo mambo ya muhimu inabidi mzazi au walezi kuwekeza kwa mtoto, ikiwemo kupenda kujisomea vitabu ili kumsaidia kuongeza uelewa.

Wazazi wengi wanawaacha watoto wakikuzwa na luninga, hali ambayo inawapa uhuru wa kutumia mitandao ya  kijamii wakidhani kuwa ni sehemu ya kujifunza.

Utaratibu huu husababisha watoto kuishi maisha ya kuigiza kama wanavyofanya wasanii mbalimbali kulingana na jambo wanalolifuatilia.

Mtoto anayejikita katika kusoma vitabu ana utofauti mkubwa na yule anayefungiwa ndani kuangalia tamthilia.

Usomaji vitamu ni msaada mkubwa wa kupanua uelewa wa mtoto pia husaidia kumwepusha mtoto kufanya maisha ya kuigiza kama nilivyoeleza awali.

Ni muhimu wazazi wawajengea watoto maisha mema ya baadaye, kwa kuwaandalia misingi ya kupenda kusoma vitabu hii itamsaidia mtoto kupenda shule zaidi.

Hakuna mtoto anayezaliwa akiwa na uelewa wa kila jambo, bali maandalizi na maelekezo humjenga mtoto.

Ni vema mzazi amfuatilie mtoto na kujua nasoma kitabu gani, kina mjenga vipi kiakili.

Jinsi ya kumshawishi mtoto kusoma

Kwanza kabisa mzazi unapaswa kuonyesha kuwa ni mpenzi wa kusoma vitabu, Pili; msomea mtoto kitabu chenye mafunzo/ maadili mema huku akiwa anakusikiliza.

Anapoanza kukua na kujua kusoma mwenyewe unapaswa kujenga mazingira ya kumnunulia vitabu kulingana na umri wake.

Kama ameanza shule ya awali si vibaya ukamnunulia vitabu vyenye picha na maelezo mbalimbali ambayo yatamsaidia kujifunza hatua kwa hatua.

Kadri anavyozidi kukua  unapaswa kumbadilishia aina ya vitabu vya kusoma, kama mzazi una uwezo mtengenezea mwanao chumba maalumu cha kusomea ili anapotamani kusoma ajue mahala sahihi pa kusomea.

Malezi ya namna hii yatamsaidia mtoto kutojihusisha na makundi ya watoto wenye tabia mbaya  pia utamsaidia kujua vitu vingi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles