29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

MZEE WA MIAKA 76 AJA NA SHARTI JIPYA KWA MKE AMTAKAYE

 

0d6a9959
MZEE Athuman Mchambua

 

Na FARAJA MASINDE-DAR ES SALAAM

MZEE Athuman Mchambua (76), ambaye ameweka tangazo nyumbani kwake la kutafuta mke, ameongeza sharti jipya kwa mke anayemuhitaji.

Amesema licha ya kupokea simu nyingi kutoka maeneo mbalimbali nchini, lakini amewataka wanawake ambao atawafanyia usaili, hasa kwa yule ambaye atakuwa ameshinda, kutobweteka kwani atakuwa katika kipindi cha mpito cha ndoa yake.

Akizungumza wakati wa mahojiano maalumu na MTANZANIA jana nyumbani kwake Mtoni Mtongani, Dar es Salaam, mzee Mchambua alisema amefikia hatua hiyo ili kuanza kupitia majina ya wanawake zaidi ya 30 ambao tayari wamejaribu bahati ya kuolewa naye.

Alisema kuwa haoni haja tena ya kuendelea kuweka tangazo hilo kwa kuwa asilimia kubwa ya wanawake wanaojitokeza hushindwa kukidhi vigezo anavyovihitaji.

Alivitaja vigezo sita muhimu vya mwanamke anayemuhitaji kuwa ni awe mcha Mungu na mwenye kutunza watoto wake.

“Vigezo vingine awe na sifa ya ndoa, awe na sifa ya mume, awe na sifa ya kilimo, awe na sifa ya kutunza watoto na awe na sifa ya usafi wa hali ya juu.

“Tangu kuanza nimepata wanawake zaidi ya 30 ambao wanne kati yao wamefika hapa nyumbani kwangu, lakini wengine wamekuwa wakiona aibu kuja hapa moja kwa moja na hivyo wamekuwa wakitumia simu. Leo (jana) nimewafanyia usaili wanawake watano kwa simu, lakini hakuna hata aliyefuzu nusu ya vigezo, wengi wamekuwa wakiteleza sifa ya kilimo,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles