28.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mwinyi: kwanini January aweke picha ile wakati huu maji yamekorogeka?

Anna Potinus

Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi amefunguka kuhusua kitendo cha Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, ckuweka picha aliyopiga naye katika ukurasa wake wa ‘twitter’ mara tu baada ya kutenguliwa uwaziri na Rais John Magufuli jana jumapili Julai 21, ambapo amesema haikuwekwa kwa wakati sahihi.

Katika picha hiyo, ambayo January aliiweka muda mchache baada ya rais kutengua uteuzi wake ikimuonyesha yeye na Mwinyi wamekaa kwenye viti viwili tofauti, ambapo aliandika;
“Kwa kweli nimeyapokea mabadiliko yaliyofanywa kwa moyo mweupe kabisa kabisa. Nitasema zaidi siku zijazo.”

Mwinyi amesema hakuona ubaya wa picha ile na wala hakuchukizwa nayo kwa sababu watu wengi wanaokwenda kumuona humuomba picha ya ukumbusho lakini kilichomshangaza ni kitendo cha kutumia picha hiyo katika kipindi hichi.

“Kwa kweli sikupenda kuona picha ya namna ile katika mazingira haya, ile ni picha ya kawaida maana watu wengi wanakuja kuniona na tukishamaliza kuzungumza wanasema tupate ukumbusho na tumefanya sana kwa mtu mmoja mmoja na kwa watu wengi sana kwahiyo nimestaajabu nilipoona imewekwa wakati huu.

“Kijana yule amendika kitabu na aliniomba nimsaidie kuandika dibaji, inawezekana alifanya kama kushukuru lakini silaumu wala sioni vibaya ila kwanini ikawe katika mazingira haya wakati maji yamekorogeka.

”Ile picha ni ya zamani lakini mambo yametokea leo na huko zamani tulikuwa na sababu ya kufanya hivyo kwasababu na mimi nilishika nafasi hii lakini pia kulikuwa na uhusiano wa kitabu chake alichokiandika maana si cha sasa hivi kiliandikwa zamani lakini kwanini ikawa sasa hivi hili kidogo limenishtua,” amesema Mwinyi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles