25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mchota maji aopoa millioni 15 kutoka CBA, Vodacom Miaka Mitano ya Mpawa

Mwandishi wetu

Mjasiriliamali anayejihusisha na biashara ya kuuza maji Mkoa wa Geita, Adrisa Martina (27), mwishoni mwa wiki aliibuka mshindi katika promosheni ya Miaka mitano ya M-Pawa na kuondoka na kitita cha fedha taslimu milioni 15.

Zawadi hiyo ilitolewa na Banki ya Biashara (CBA), kwa kushirikiana na Vodacom Tanzania katika Promosheni ya kusherehekea maadhimisho ya miaka mitano ya M-Pawa iliyohudhuriwa na Naibu Gavana Mkuu wa benki Kuu ya Tanzania, Bernard Kibesse, Mkurugenzi Mkuu wa CBA Tanzania Gift Shoko, wasimamizi wa Vodacom, wafanyakazi wa CBA pamoja na timu ya M-pawa ambapo sherehe hizo zilimalizwa kwa washindi wa gofu walioshiriki mashindo ya kuadhimisha miaka mitano ya m pawa kupatiwa zawadi lukuki.

Akizungumza katika hafla hiyo Naibu gavana aliwashukuru CBA na Vodacom kwa huduma zao nzuri ambapo alimpongeza Andrisa Mathias kwa ushindi alioupata.

Baada ya kukabidhiwa zawadi hiyo, Adrisa alisema amefurahi sana kuwa mmoja wa wateja wenye bahati ya kujishindia fedha hizo na kuwashukuru CBA pamoja na Vodacom kwa kufanikisha ndoto zake. 

“Ninaahidi kuzitumia fedha hizi vizuri na nitaitumia kuzalisha zaidi kwenye biashara zangu na  sitoacha kutumia huduma za M-Pawa,” amesema Adrisa

Kwa upande wa Mkurugenzi Mtendaji wa CBA, Gift Shoko, alisema lengo la benki hiyo lilikuwa kumgusa kila mwanachi na asie na akaunti ya benki na hilo litabaki kuwa lengo la CBA pamoja na M-pawa bila kusahau kutunza fedha ikiwamo na kuongeza mfumo wa maisha ya wafanyabiashara wadogo wadogo nchini.

“Tulivyo anza miaka mitano iliyopita tulikuwa na wateja wanne tu wa M-pawa na mpaka sasa tumefanikiwa kufikisha wateja millioni 8.5, hii inanipa uwezo mkubwa wa kuvipongeza vyama vyote vilivyo shiriki na kufanikisha malengo haya ikiwamo Vodacom, Serikali, wateja wetu wote wa M-pawa na kila aliyeshiriki kwenye zoezi hili na kutusaidia kufika mahali hapa,” alisema Shoko.

Aliongeza kuwa M-pawa imewasaidia wa Tanzania wengi kubadilisha mfumo ya maisha yao na haswa wafanya biashara wadogo wadogo ambao wanaendelea kuhifandhi pesa zao na kuchukua mikopo inayowasaidia kuboresha biashara zao bila kusahau pesa hizo zinaleta ulinzi katika mahitaji yao ya ghafla.

“Mtu yoyote anaweza kukopa popote alipo na muda wowote akiwa na M-pawa na fedha za wateja wetu zina ulinzi, bila yakua na malipo ya ziada,” Alisema Shoko 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles