Mwijage kuwa mgeni rasmi fainali Maisha Plus

0
644
Charles Mwijage
Charles Mwijage
Charles Mwijage

Na HADIA KHAMIS –DAR ES SALAAM

WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage, amekubali kuwa mgeni rasmi katika fainali ya Maisha Plus Afrika Mashariki 2016.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwijage alisema atahudhuria katika kijiji hicho na atafanya uzinduzi wa mashine ya kukobolea mahindi.

Alisema amepata mwaliko wa kwenda katika Kijiji cha Maisha Plus na kazi kubwa ambayo ataifanya ni kuzindua mashine.

Mbali na uzinduzi huo, Mwijage atamkabidhi mshindi wa Maisha Plus msimu wa tano kitita cha Sh milioni 30.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here