24.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mwenyekiti UVCCM Iringa ajiuzulu

MWENYEKITINa Aziza Masoud, Dar es Salaam
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Mkoa wa Iringa, Tumaini Msowoya, amejiuzulu nafasi yake kwa kile alichodai kuepuka mgongano wa masilahi.

Amesema amefikia hatua hiyo baada ya mume wake, Frank Kibiki kutangaza nia ya kuwania ubunge wa Iringa Mjini, huku akihisi kutotenda haki katika vikao vya chama ambavyo huwa na uamuzi.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Tumaini, ilieleza kuwa ameamua kuchukua hatua hiyo ili aweze kutenda haki katika uteuzi wa wagombea wengine.

“Hili nililizingatia kwamba kuwamo kwenye vikao hivyo nisingeweza kutenda haki kwa wagombea wengine na hivyo kutotimiza wajibu wangu kikanuni na kikatiba katika kusimamia haki za wagombea wote na si vinginevyo,” alisema Msowoya.

Alisema anaamini baada ya tukio hilo atapata nafasi na uhuru mkubwa wa kushiriki katika harakati za kupata viongozi wazuri kutoka chama hicho kwakutumia utaratibu wa kikatiba kama ilivyo kwa wanachama wengine.

Mwenyekiti huyo wa UVCCM, aliwashukuru vijana na wanachama wote wa CCM wa Mkoa wa Iringa kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chote akiwa kiongozi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles