32.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mwendokasi kukamilisha mfumo tiketi kieletroniki

Na Mwandishi wetu – Dodoma

WAKALA wa mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam (DART),  unakamilisha utengenezaji wa mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa nauli utakaosaidia kupunguza msongamano kwenye vituo.

Hayo yalielezwa jana bungeni na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), wakati ikijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu, Aysharose Matembe (CCM).

Katika swali lake Aysharose alidai uamuzi wa Serikali kutengeneza miundombinu ya usafiri wa mabasi ya mwendokasi ulilenga kuondoa kero kwa wananchi jijini Dar es Salaam, lakini usafiri huu umekuwa kero kubwa kwa watumiaji ikiwemo kujaza abiria bila kujali athari.

Aysharose alihoji Serikali ina mpango gani wa kudhibiti ujazaji abiria pamoja na kuweka utaratibu mzuri kwa watumiaji wake.

Ikijibu swali hilo, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) ilieleza kuwa  ili kupunguza msongamano wa abiria, DART inaendelea na taratibu za ununuzi ili kumpata mzabuni atakayeongeza idadi ya mabasi kutoka 140 yaliyopo sasa hadi 305.

Wizara ilieleza kuwa wakala unakamilisha utengenezaji wa mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa nauli na kuongozea utakaosaidia kupunguza msongamano kwenye vituo kwani abiria wataweza kupata taarifa za mabasi kwa wakati na hivyo kupanga safari zao kwa ufasaha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles