Mwasiti: Mwaka huu ni kazi tu

0
1151

mwasitiNA THERESIA GASPER

STAA wa muziki wa Bongo Fleva akitokea Jumba la Vipaji Tanzania ‘THT’, Mwasiti Almasi, amesema mwaka huu amejipanga kikazi zaidi ili kuwapa burudani mashabiki wake.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Mwasiti alisema amejipanga kuachia video tatu mwaka huu huku zikiwa kwenye kiwango cha hali ya juu japokuwa zitafanyiwa nchini Tanzania.

“Nimekaa kimya kipindi kirefu na najua mashabiki wangu watakuwa wamenimisi, hivyo nawaomba Watanzania kwa ujumla wakae tayari mwaka huu kupokea mambo mazuri zaidi kwani ni mwendo wa kazi tu,” alisema Mwasiti.

Mwanadada huyo ambaye ni zao la THT amefanikiwa kufanya vyema kwenye baadhi ya nyimbo zake kama Hao, Sio kisa pombe, Sema naye, Mapito na nyingine nyingi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here