22.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

MWAROBAINI WATHIBITIKA KUUA WADUDU WA PAMBA

pamba

Na SAMWEL MWANGA,

WAKULIMA wa   pamba nchini hususan wa Kanda ya Ziwa  huenda wakaondokana na adha ya kupatikana kwa madawa mahususi ya  kuua wadudu wanaoshambulia zao hilo baada ya kugundulika kwa mmea wa mwarobaini kuwa mbadala wa dawa nyingine.

Awali wakulima wa  pamba nchini walikuwa wameshindwa kupata suluhisho la madawa ya kuua wadudu ambayo yalikuwa yakisambazwa.

Madawa hayo yamekuwa yakibainika kutokuwa na uwezo wa kuua wadudu hali iliyosababisha wakulima wengi kukata tamaa na zao hilo.

Meneja wa Kiwanda cha Kuchambua Pamba cha Alliance  wilayani Bariadi, Boaz Ogola, alisema kwa sasa mmea huo utakuwa ni suluhisho kwa wakulima ikizingatiwa  hauna athari zozote kwa mimea na binadamu.

Alisema  dawa hiyo haina gharama yoyote kwa mkulima na hutengenezwa kwa kutwanga majani ya mwarobaini kwa
kuyaloweka kwenye maji  na kuyachuja kuondoa mabaki ya majanikabla ya kupulizia zao hilo.

“Tanzania ni nchi ya kwanza kwa kuwa na pamba ya asili na kwa sasa pamba hii ina soko kubwa.

Lakini pia mkoa unajiandaa kuzalisha bidhaa za pamba ambazo zinahitaji pamba yetu.

“Sisi kama wazalishaji tumeanza kuzalisha pamba ya asili kwa kuwapa elimu wakulima kutumia dawa za asili kunyunyuzia  kuua wadudu,”alisema.

Alisema pia kuwa  tatizo la kutokuota kwa mbegu lililokuwapo misimu iliyopita limeonekana kutoweka mmsimu huu kutokana na wakulima kuuza pamba ambayo haikuwekewa maji na mchanga wakati wa msimu uliopita.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles