24.9 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

‘HUSSEIN PAMBA KALI’ KORTINI KWA KUSHINDWA KULIPA DENI

tox-duka

Na MANENO SELANYIKA-DAR ES SALAAM

MFANYABIASHARA na mmiliki wa maduka ya nguo jijini Dar es Salaam, Hussein Mkangala (38), maarufu ‘Hussein Pamba Kali’ amefunguliwa kesi ya madai katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kinondoni akidaiwa kushindwa kulipa Sh milioni 75 alizokopa kutoka kwa Anna Kiabi.

Shauri namba 146/2016 kwa mara ya kwanza lilitajwa jana katika mahakama hiyo ambapo upande wa mdai ulikuwa unasimamiwa na Wakili Jonas Nkya, wakati ule wa utetezi (mdaiwa) ukiongozwa na wakili wa kujitegemea  Ernest Swai.

Mbele ya Hakimu Is -Haq Kuppa, Wakili Nkya alidai mahakamani hapo kwamba tukio hilo lilitokea Novemba 20 mwaka jana ambapo mfanyabiashara huyo alikopeshwa Sh milioni 80 kwa ajili ya kuendeleza shughuli zake za kibiashara, lakini hakuweza kurejesha.

Wakili huyo aliongeza kwamba ilipofika Mei 22 mwaka huu mdaiwa ambaye ni Husseni alimtuma mdogo wake aitwaye Hassan Mkangala, apeleke Sh milioni 5 kwa Anna na kiasi kilichobakia hajalipa tena hadi sasa.

Upande wa utetezi uliiomba mahakama hiyo iwape muda wa siku 6 ili waweze kujibu madai ya walalamikaji.

Hakimu Kuppa aliahirisha shauri hilo hadi Desemba 15 mwaka huu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles