30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanri ateuliwa kuwa balozi wa pamba nchini

Na Derick Milton, Busega

Bodi ya Pamba nchini imemtangaza aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Aggrey Mwanri, kuwa Balozi wa pamba nchini ambapo kazi yake kubwa itakuwa ni kuhamasisha wakulima wa zao hilo kuzalisha kwa tija.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya kuongeza tija katika kilimo cha zao la pamba iliyofayika leo Jumapili Julai 4, 2021 katika Kijiji cha Kijereshi Wilayani Busega mkoani wa Simiyu.

Mkurugenzi wa Bodi ya pamba nchini, Marco Mtunga, amesema kuwa bodi imemchangua Mwanri kuwa balozi kutokana na kazi kubwa ya kuhamasisha kilimo hicho katika mkoa wake kipindi akiwa Mkuu wa mkoa.

Mtunga amesema Mwanri akiwa mkuu wa mkoa wa Tabora alihamasisha kilimo chenye tija katika Wilaya ya Igunga, na kupelekea bodi kuanzisha kitalu cha mbengu bora katika wilayani humo.

Amesema mstaafu huyo atafanya kazi yakuhamasisha kampeini hiyo ya kilimo chenye tija katika zao la pamba, kwenye mikoa yote nchini ambayo inazalisha pamba.

“Kazi kubwa ya balozi huyu, itakuwa kuhamasisha wakulima kuzalisha kwa tija kwa kufuata kanuni bora 10 za kilimo cha pamba, kazi ambayo ataianza kuanzia sasa hadi mwezi Novemba mwaka huu,” amesema Mtunga.

Amesema kuwa katika kampeini hiyo, wakulima watahamasishwa kuweka mbolea ya samadi wakati wa kupanda, kutumia kanuni mpya ya vipimo ya 60 kwa 30 lengo likiwa kuzalisha kutoka kilo 200 hadi 1000 kwa hekari moja.

Upande wake, Mwanri ameishukuru bodi ya pamba kwa kumteua kuwa balozi, ambapo ameeleza atafanya kazi hiyo kwa kiwango kikubwa ili kuweza kufikia malengo ambayo yamewekwa.

Amewataka wadau wote katika kilimo cha pamba, wakiwemo viongozi wa serikali na siasa ngazi zote kutoa ushirikiano katika mapinduzi hayo huku akiwataka wadau wote kushirikiana katika kampeini hiyo ya kuhamasisha wakulima.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles