25.8 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 16, 2024

Contact us: [email protected]

Kondoa kutambua na kuendeleza vipaji vinavyotoka maeneo ya vijijini

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

Wilaya ya Kondoa imepanga kuvitambua na kuviendeleza vipaji vinavyotoka katika maeneo ya vijijini kupitia Ligi ya Soka ya Wilaya hiyo ambayo inatarajiwa kuanza kesho katika uwanja wa Sabasaba Wilayani humo ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Wilaya hiyo, Dk. Khamis Athumani Mkanachi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jumamosi Julai 3, 2021, Mwenyekiti wa Chama cha Soka Wilaya ya Kondoa, Msekela Majuto amesema wameamua kuanzisha ligi hiyo ambayo uzinduzi wake  unatarajiwa kufanyika kesho katika uwanja wa Sabasaba Wilayani humo ambapo amedai ligi hiyo  imegawanyika katika makundi mawili.

“Lengo ni kutafuta timu ya Kondoa Combine ambayo pia itajumuisha vipaji kutoka katika maeneo ya vijijini timu hiyo  itashiriki  mashindano ya Azam Confederation Cup ambayo inatarajiwa kuanza hivi karibuni  na itakuwa ni timu ambayo itajumuisha Halmashauri zote mbili kupitia mashindano haya tutachagua wachezaji lakini pia tutajikita kuboresha viwanja,”amesema.

Amesema wamejikita zaidi katika maeneo ya vijijini ambapo hatua ya kwanza ligi hiyo itakuwa na vituo katika tarafa za Lyoli, Serya Sabasaba, Mahongo Ulolimo, Loo na Kisese.

Amesema kila bingwa katika kituo atashiriki hatua inayofuata na kisha  fainali ya ligi hiyo inatarajiwa kufanyika Agosti 15 mwaka huu ambapo wamepanga hatua ya makundi imalizike Julai 21 mwaka huu  

“Tumeamua kila bingwa atakaepatikana atapewa zawadi ya jezi ambaye atakuja kushiriki hatua ya fainali, itahusisha timu nane zawadi ya mashindano ni Sh 700,000 na mshindi  wa pili atapata Sh 300,000 na  ushirikiano upo kwa Mbunge wa Jimbo la  Kondoa,Ally Makoa ambaye  ametupa zawadi  za washindi na  mdau Omari Kimbisa yeye ametoa  jezi za waamuzi,”amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles