27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mwandishi mkongwe Marekani afariki dunia

WASHINGTON DC, MAREKANI



MWANDISHI mkongwe nchini hapa na rais wa zamani wa Kampuni ya vichekesho ya  Marvel Comics,  Stan Lee, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95.

Mwaka 1961, Lee alibuni filamu nne bora za Marvel Comics na kuzipatia majina maarufu ikiwemo Spider-Man na The Incredible Hulk.

Kwa mujibu wa wakili wa familia yake, mwandishi huyo mkongwe wa vitabu vya vichekesho alifariki dunia katika kituo cha matibabu cha Cedars Sinai kilichopo mjini Los Angeles.

Ofisa Mkuu Mtendaji wa Kampuni ya burudani ya Pow inayomilikiwa na Lee, alimtaja kama baba wa mitindo ya pop kwa kubuni wahusika wanaofahamika kote duniani.

Mkurugenzi Mkuu Shane Duffy alimkumbuka kama mwanzilishi wa kweli ambaye hana mpinzani.

Akizungumza na mtandao wa TMZ unaoangazia habari za watu mashuhuri, binti yake, JC Lee alisema baba yake alikuwa mtu mashuhuri na mwenye heshima.

Binti huyo pia aliliambia Shirika la Habari la Uingereza – Reuters kwamba katika utendaji kazi wake alihisi kuwa na wajibu mkubwa kwa watu.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, miaka ya hivi karibuni, Lee amekuwa akiiugua mara kwa mara.

Lee alifahamika kwa kutengeneza filamu maarufu alipokuwa na kampuni ya filamu ya Marvel, japo aliachana na kampuni hiyo mwaka 1972.

Siku ya Jumapili, ambayo ni siku ya kuwatambua mashujaa, ukurasa wake rasmi wa Facebook uliweka picha zake akiwa jeshini, na kuandika kwa utani kwamba alikuwa mtunzi wa michezo tangu wakati wa vita ya pili ya dunia.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles