DERA, Pakistan
Watu tisa wamefariki na wengine 30 kujeruhiwa nchini Pakistan baada ya mwanamke mmoja kujitoa muhanga na kujilipua kwa bomu nje ya hospitali moja nchini humo.
Tukio hilo limetokea leo Jumapili Julai 21, wakati majeruhi kadhaa wa shambulio la awali dhidi ya polisi wakifikishwa hospitalini hapo.
Ofisa Mwandamizi wa Jeshi la Polisi wa jimbo la Dera Ismail Khan, Salim Riaz Khan, amethibitisha kutokea tukio hilo ambapo amesema watu hao walijeruhiwa na mtu mwenye silaha aliyekuwa katika pikipiki alipofyatua risasi katika makazi ya polisi na kuwauwa wawili.
Ofisa huyo amesema katika tukioa la kujitoa muhanga mwanamke huyo askari polisi wengine wanne na raia wawili walifariki.
Aidha kundi la wapiganaji la Taliban, limedai kuhusika na shambulio hilo ingawa halijasema kuwa mwanamke ndiye aliyehusika na mashambulizi na katika miaka ya hivi karibuni, jeshi la Pakistan limekuwa likiendesha operesheni kabambe dhidi kundi ya kundi hilo na makundi mengine ya wapiganaji katika eneo la mpaka wake na Afghanistan.