26.9 C
Dar es Salaam
Friday, January 3, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Mwanamke ajifungua baada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi

 NEW DELHI, India



MWANAMKE mmoja nchini hapa, Meenakshi Valand, amejifungua mtoto  baada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi.

Valand alijifungua mtoto mwezi uliopita na anakuwa miongoni mwa wanawake wachache ambao walifanikiwa kupata mtoto baada ya kupandikizwa mfuko huo.

“Sikuweza kujizuia kulia baada ya kusikia sauti ya mwanangu akilia. Haya ni machozi ya furaha – Nimepoteza watoto sita katika miaka kadhaa iliyopita,” Valand aliliambia Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).

Mama huyo wa miaka 28-alijifungua mwezi uliopita nchini India baada ya kupandikizwa mfuko wa uzazi wa mama yake mzazi.

Katika miaka tisa ya ndoa yake,  Valand alizaa watoto wawili waliofariki dunia.

Alipoteza wengine wanne katika uja uzito, hatua iliyomsababisha kukatika mfuko wake wa uzazi.

Hata hivyo hakukata tamaa kwa kile anachodai alikuwa akihitaji kupata mtoto wake  mwenyewe na hakutaka kutumia mbinu nyingine yoyote.

Kwa mujibu wa jarida la mataifa la utafiti wa sayansi, asilimia 15  ya watu hawana uwezo wa kuzaa na watatu  kati ya asilimia  tano ya matukio hayo husababishwa na matatizo ya mfuko wa uzazi.

Mwanamke huyo alitimiza ndoto zake baada ya kumtembelea Dk. Shailesh Putambekar ambaye ni mtaalamu wa upasuaji na upandikizaji wa mfuko wa uzazi katika Hospitali ya Galaxy Care iliyopo mjini Pune.

Wakati huo mama yake, Sushila Ben alikuwa amejitolea kumpatia mfuko wake wa uzazi ili kumuwezesha kupata mtoto.

Upandikizaji huo ulifanywa na kundi la wataalamu 12 mwezi Mei mwaka jana  na ulifanikiwa, lakini Januari mwaka huu alikabiliwa na changamoto nyingine baada ya hatua ya kuhamisha kijusi kukwama.

Hata hivyo utaratibu huo ulifanywa tena  Aprili mawaka jana  na wiki 20 baadaye mwanawe Radha alizaliwa kabla ya kufikisha wakati wa kuzaliwa akiwa na kilo 1.45.

Upandikizaji wa mfuko wa uzazi umefanywa katika mataifa 10 zikiwemo Sweden, Saudi Arabia, Uturuki, Marakani, Uchina na Jamhuri ya Czech, Brazil, Ujerumani, Serbia na India.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles