Jeshi lawasili mkoani Mtwara kusomba korosho

0
1732

Nora Damian, MtwaraAgizo la Rais John Magufuli la kununua korosho zote limeanza kutekelezwa ambapo tayari Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limewasili mkoani Mtwara kwa kazi hiyo.

Mapema leo asubuhi askari wa JWTZ wamewasili wilayani Newala na kuanza kukagua maghala ya kuhifadhia korosho yaliyopo wilayani humo.

Askari hao ambao waliongozana na Mkuu wa Wilaya hiyo, walitembelea na kukagua maghala matatu yaliyopo wilayani humo ambayo ni Micromix, Agro Focus na ghala la Chama Kikuu cha Ushirika cha Tandahimba na Newala ( Tanecu).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here