24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, April 14, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanafunzi aacha shule ageukia uganga wa kienyeji

Na SAMWEL MWANGA – MASWA

MWANAFUNZI wa darasa la tano Shule ya Msingi Mwabulimbu mwenye umri wa miaka 15 (jina linahifadhiwa), anadaiwa kuacha shule na kujikita kutoa tiba ya jadi kwa kutibu magonjwa mbalimbali katika Kijiji cha Mwaliga wilayani Maswa.

Akizungumza na MTANZANIA kijiji hapa jana, mwanafunzi huyo alisema amefurahia kazi kwa sababu anaimudu vizuri kwa kupata wagonjwa wengi ambao amekuwa akiwahudumia kwa malipo ya fedha na au kupewa mifugo.

Alisema amekuwa akijihusisha na shughuli hizo, tangu akiwa darasa la tatu kupitia kwa jirani yao ambaye alikuwa mganga wa jadi. Hivi karibuni alihama kijijini hapo na kwenda Kijiji cha Namanyere Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa.

Alisema shule zilipofungwa kutokaka na uwapo wa ugonjwa wa corona, alipata nafasi ya kuendeleza shughuli hizo baada ya kupata taarifa kuwa kuna wagonjwa wa

magonjwa mbalimbali katika kijiji hicho wanahitaji kutibiwa.

“Wakati wa likizo ya ugonjwa wa corona, shule zilifungwa muda mrefu, nilikuwepo nyumbani,akuna shughuli za kufanya,nilipata taarifa kuna wagonjwa wanasumbuliwa na ugonjwa wa kuvimba tumbo hapa kijijini, niliaaga nyumbani nikatafute fedha, nikaniruhusiwa ila walishangaa,nimekuwa mganga na umri wangu huu mdogo.

“Nilipofika kule nilipokelewa,niliweza kuwatibu wagonjwa wanne, nililipwa fedha na ng’ombe wanne, nilipewa nyumba kwa ajili ya kuendeleza kazi yangu ambayo naiheshimu mno kwa sababu inasaidia kuwaponya wagonjwa,”alisema.

Alisema dawa anazotumia kuwatibu wagonjwa wake, ni mizizi ya miti na wala hapigi ramli na kusisitiza dawa zake zimekuwa na mafanikio makubwa kutokana na kupata wagonjwa mbalimbali kutoka nje ya wilaya hiyoa.

Mmoja wa maofisa elimu msingi katika wilaya hiyo ambaye hakupenda kutaja jina lake

kwa kuwa si msemaji, alisema mwanafunzi huyo ambaye kwa sasa ameacha shule ni miongoni mwa wanafunzi ambao hajarudi shuleni kuendelea na masomo baada ya shule kufunguliwa Julai, mwaka huu.

“Wakati wa janga la ugonjwa wa corona,Serikali ilifunga shule kuanzia shule za awali hadi vyo vikuu, wanafunzi walikuwa huru,wengine wakajiingiza katika shughuli mbalimbali kama huyo ambaye ameamua kuwa mganga wa jadi,”alisema.

Mkuu wa Wilaya ya Maswa,Aswege Kaminyoge alisema wilaya imejipanga kuhakikisha watu wote waliowasababishia watoto kutoendelea na masomo wanasakwa na kuchukuliwa za kisheria.

“Tumejipanga kuhakikisha watu wote ambao waliwasababishia watoto wao kutorejea shule kuendelea na masomo wanasakwa na kuchukuliwa hatua,tutaendelea kuwatafuta wanafunzi wote ambao hawajarudi tangu shule zifunguliwe baada ya ugonjwa wa corona kudhibitiwa,”alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles