24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

Watanzania hawajafikia kiwango ulaji nyama-Serikali

Na ELIZABETH KILINDI – NJOMBE

KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk.Rashid Tamatamah amesema Watanzania hawajafikia kiwango cha kimataifa cha ulaji wa nyama ambacho ni kilo 50 kwa mtu mmoja kwa mwaka.

Pia amesema changamoto nyengine, ni unywaji wa maziwa ambapo kila mtu anatakiwa angalau anywe lita 200 kwa mwaka.

Tamatamah aliyasema hayo juzi, wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambayo kitaifa yanafanyika mkoani Njombe,yakiwa na kauli mbiu ‘kesho njema inajengwa na lishe bora endelevu’.

Alisema kwa mujibu wa Shirika

la Kilimo na Chakula la Umoja wa Mataifa (FAO), viwango vya ulaji nyama na unywaji wa maziwa nchini bado uko chini.

‘’Bado ulaji wa nyama na unywaji wa maziwa si wa kuridhisha, natoa

kutoa rai kwa wananchi kuongeza ulaji wa nyama ili tuweze kufikia

kiwango hiki ambacho kinatambulika kimataifa,’’alisema.

Alisema mwaka 2019/20, uzalishaji wa maziwa umefikia lita bilioni 3, ikilinganishwa na lita bilioni 2.7 zilizozalishwa mwaka 2018/19.

‘’Ongezeko la uzalishaji linatokana na ongezeko la ng’ombe pamoja na kuboreshwa mazingira ya uwekezaji katika tasnia ya

maziwa nchini,’’alisema.
Naibu Waziri wa Kilimo,

Omari Mgumba alisema Tanzania inakabiliwa na tatizo la uwapo wa ongezeko la viribatumbo kwa wanawake kutokana na kutozingatia mlo kamili.

Aliwataka wananchi mkoani Njombe kuacha imani potofu, kuwa mtoto akikosa lishe amebemendwa.

“Hakuna kubemendwa, ni kukosa lishe,kuna mila potofu eti mtoto akikosa lishe kabemendwa, acheni hizo imani, jueni amepata utapiamlo,”alisema Mgumba.

Kwa upande wa mkuu wa mkoa wa Njombe Marwa Rubirya alisema ili kupambana utapiamlo tayari mkoa umepanga mikakati mbalimbami ikiwemo kutoa elimu kwa wananchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles