33.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, February 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mwana FA: Msanii kukaa kimya ni heshima

MWANAFANA JENNIFER ULLEMBO
WAKATI wasanii wengi wa Bongo Fleva wakifikiria kutoa nyimbo zao mfululizo, msanii mwenzao, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA’ anaendelea kutunza heshima yake kwa kutokutoa wimbo kwa muda mrefu.
Mwana FA aliliambia MTANZANIA kwamba, msanii kuwa kimya si kuishiwa mashairi bali ni hali ya kutunza heshima yako kwa mashabiki.
Alifafanua kwamba, idadi kubwa ya wasanii wanaofanikiwa katika muziki huo hutumia muda mwingi kufikiria vitu vipya ili kuboresha kazi zao tofauti na wanaokurupuka kutoa wimbo kwa muda mfupi.
“Unajua mashabiki wamekuwa na fikra potofu, wanapoona msanii yupo kimya akili zao zinawatuma kwamba kaishiwa wakati sivyo,” alisema Mwana FA.
Aliongeza kwamba, kukurupuka mara nyingi kumekuwa kukimaliza vipaji vya wasanii kwa haraka na kujikuta hawadumu kwenye fani zao huku akidai yupo katika maandalizi ya wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Sitoiela’.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles