24.8 C
Dar es Salaam
Friday, September 29, 2023

Contact us: [email protected]

Baby Madaha: Ubunifu unahitajika kwa wachekeshaji

babayNA GEORGE KAYALA
MWIGIZAJI wa filamu za Bongo, Baby Madaha, amesema ubunifu kwenye kazi za sanaa hasa za uchekeshaji ni jambo la msingi kuzingatiwa kwa kuwa wasanii wengi wa filamu za vichekesho wamekuwa wakilipua kazi zao na kuchosha watazamaji.
“Suala la ubunifu kwenye kazi za sanaa ni jambo la msingi, inatakiwa shabiki akiangalia filamu ya vichekesho asichoke kuiangalia maana haitakuwa na maana kama filamu ya vichekesho, lakini mtu anaitazama mwanzo hadi mwisho amekasirika badala ya kumchekesha,’’ alieleza.
Madaha aliongeza kwamba, ametoa kauli hiyo baada ya kuona mabadiliko katika moja ya filamu za vichekesho iliyopewa jina la ‘Kibonge Mdudu’ ambayo ipo sokoni kwa sasa.
“Uigizaji wa vichekesho unatakiwa kuwa kama, Martin White ‘Tini White’, Jacob Mkweche ‘Ringo’ na Charles Mkangwa walivyoigiza vitu vipya ambavyo havijazoeleka kama wachekeshaji wengine wanavyofanya katika filamu na maigizo yao,” alimaliza Baby Madaha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles