23.2 C
Dar es Salaam
Saturday, July 27, 2024

Contact us: [email protected]

Mwalimu Mkuu mbaroni kwa rushwa

CHRISTINA GAULUHANGA Na BOSCO MWINUKA (TURDACO) –Dar es salaam

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) Mkoa Temeke, imemkamata Mwalimu Mkuu wa Shule ya Awali na Msingi Real Hope iliyopo Mbagala Majimatitu, Dar es Salaam, Ayubu Mtondo kwa kosa la  kuomba na kupokea rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Naibu Mkuu wa Takukuru, Ramadhani Ndwatah, alisema mwalimu huyo alipokea Sh 100,000 ili kumsaidia kumrudisha kazini mtumishi mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa.

Ndwatah alisema Februari 28, mwaka huu, saa 11 jioni,  mwalimu huyo akiwa ofisini kwake, alipokea fedha za mtego ili aweze kumsaidia mtumishi wake aliyesimamishwa kazi kurudi kazini.

“Mwalimu Mtondo anakabiliwa na makosa ya kuomba na kupokea rushwa kinyume na kifungu cha 15 cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2017,” alisema Ndwatah.

Alisema uchunguzi dhidi ya tuhuma hizo umekamilika na mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa mahakamani na kufunguliwa mashtaka kwa kosa la kushawishi kuomba na kupokea rushwa.

Alitoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za vitendo vya rushwa kupitia mitandao yote ya simu kwa kupiga au kutuma ujumbe mfupi namba 113.

Alisema taasisi hiyo itaendelea kufanya kazi kwa weledi ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote wanaojihusisha na vitendo hivyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles