26.2 C
Dar es Salaam
Monday, March 27, 2023

Contact us: [email protected]

Njaa yaikumba Zimbabwe

HARARE, ZIMBABWE

ZAIDI ya watu milioni tano nchini Zimbabwe, karibu theluthi ya watu wote nchini humo wanahitaji msaada wa chakula.

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP)  limeanzisha mchakato wa kuomba msaada wa dola milioni 331  kwa ajili ya kuisaidia nchi hiyo kupambana na athari ya ukame, kimbunga na mdororo wa uchumi.

Kiongozi wa WFP, David Beasley, alisema watu wengi wapo kwenye dharura ya njaa.

Zimbabwe ambayo imepata kuwa Taifa linalojitosheleza kwa chakula lakini kwa miaka mingi imejikuta katika hali mbaya.

Mavuno ya sasa yameathiriwa na ukame pamoja na bei ya chakula ambayo imepanda haraka.

Upungufu wa maji pia umeathiri hali ya upatikanaji wa umeme nchi nzima.

Nchi hiyo pia inakabiliwa na mdororo wa  fedha licha ya kutoa dola ya Zimbabwe nyingine muongo mmoja baada ya kukubwa na mfumuko mkubwa wa bei.

“Tunazungumzia watu ambao wanapambana na njaa kama hatupo hapa kuwasidia,” alisema kiongozi huyo wa WFP na kuongeza;

“Tunakabiliwa na ukame wa aina yake  ambao hatujapata kuuona kwa miaka mingi,” alisema

Ukame huo umesababisha maji kupungua katika bwawa la Kariba, na kuathiri uzalishaji wa umeme.

Matatizo hayo yanayoshuhudiwa sasa Zimbabwe msingi ni kimbunga cha Idai ambacho kiliikumba nchi hiyo mapema mwaka huu.

Kimbunga hicho kikubwa kiliathiri pia baadhi ya sehemu nchini Malawi na Msumbiji na hivyo kuathiri Wazimbabwe takribani 570,000 na kuwaacha maelfu bila makazi.

Wiki iliyopita Waziri wa Fedha wa Zimbabwe,  Mthuli Ncube  alisema tangu Januari Serikali ilitoa nafaka kwa ajili ya familia 757,000 vijijini na mijini.

Juzi Jumanne Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa, ambaye alichukua madaraka kwa kutoka kwa kiongozi aliyetawala muda mrefu  nchini humo Robert Mugabe Novemba 2017,  alitangaza ukame kama janga la kitaifa.

Umoja wa Mataifa (UN) tayari umetoa dola milioni 294 kwa ajili ya Zimbabwe lakini unasema unahitaji msaada zaidi wa fedha kwa kuwa athari ya ukame imeenea sehemu kubwa nchini humo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,206FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles