23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Mwalimu Mkuu matatani kwa wizi wa mitihani ya darasa la nne

Na Derick Milton, Simiyu

Jeshi la polisi Mkoa wa Simiyu linamshikilia Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Shimbale iliyoko Halmashauri ya Mji wa Bariadi, Gaudensia Anyango (45) kwa tuhuma za kufanya udanganyifu katika Mtihani wa taifa wa Darasa la Nne.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Ofisini kwake, Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa ACP Shadrack Masiji, amesema Mwalimu huyo alikamtwa Oktoba 28, 2021 saa 5:30 Asubuhi wakati wanafunzi hao wakifanya mtihani wa Kiswahili na Hisabati.

ACP Masiji amesesma kuwa Mwalimu huyo aliwachukua wanafunzi wa darasa tano na Sita kwa ajili ya kuwafanyia mitihani wenzao 23 ambao ni watoro katika shule hiyo.

“Wasimamizi wa mtihani waligundua uwepo wa wanafunzi wanaofanya mtihani huo lakini siyo wahusika, ndipo walipoanza uchunguzi na kugundua wanafunzi 23 siyo darasa la nne,” amesema ACP Masiji na kuongeza kuwa;

“Lengo la Mwalimu huyo ni kutaka shule yake ifanye vizuri na aweze kupata zawadi pindi matokeo yatakapotoka, wale wanafunzi ambao walifanyiwa mtihani ilibainika kuwa ni watoro wa muda mrefu,” ameongeza ACP Masiji.

Kamanda huyo amesema kuwa Mtuhumiwa yupo Mahabusu anaendelea kuhojiwa kuhusiana na tuhuma hizo na mara baada ya upelelezi huo kukamilika jalada litafikishwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua za sheria na kufikishwa mahakamani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles