26.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mwalimu aliyemuingilia Mwanafunzi Dar apandishwa kizimbani

Na Faraja Masinde, Mtanzania Digital

Mwalimu wa kujitolea na mkazi wa Mwanamtoti Mbagala Dar es Salaam, Ally Said Kaule maarufu Sir Ally(26) amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Wilaya ya Temeke kwa kosa la kumuingilia kingono.

Akisomewa hati ya mashtaka leo Jumanne Oktoba 11, 2022 mbele ya Hakimu Mkazi Aziza Mbajo, Mwendesha Mashtaka wa Jamhuri, Grace Lwila amedai kuwa katika tarehe isiyojulikana Agosti, mwaka huu eneo la Mbagala Mwanamtoti mshtakiwa alimuingilia kingono mtoto wa miaka (11) jina linahifadhiwa.

Mshtakiwa amekana kutenda kosa hilo mbele ya mahakama na Mwendesha mashtaka amedai upelelezi umekamilika 

Hakimu Mbajo amesema dhamana kwa mshtakiwa ipo wazi kwa masharti ya kuwa na wadhamini wawili waaminifu watakao saini bondi ya Sh milioni 3 kila mmoja.

Hata hivyo, mshtakiwa amerudishwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti ya dhamana na kesi hiyo namba 551 ya mwaka 2022 itatajwa tena Oktoba 25, mwaka huu.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka Sir Ally ambaye ni Mwalimu wa kujitolea katika Shule ya Msingi Mbagala Kuu wilayani Temeke, Dar es Salaam katika tarehe isiyojulikana Agosti, mwaka huu alimuingilia kingono mtoto huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles