30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, May 23, 2024

Contact us: [email protected]

Maabara ya Mkemia Mkuu kuongeza maabara Kanda ya Kati na Kusini

Na Ramadhan Hassan, Dodoma

MAMLAKA ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali imesema imepanga kuongeza maabara nyingine katika Kanda ya Kusini (Mtwara) na Kanda ya kati (Dodoma) ambapo Sh bilioni 8.14 zitatumika katika ujenzi huo.

Aidha imesema vibali vya uingizaji wa kemikali nchini vimeongezeka kutoka 49,234 mwaka wa fedha 2020/21 hadi kufikia 63,588 katika mwaka wa fedha 2021/2022.

Hayo yameelezwa leo Oktoba 11 mwaka huu jijini hapa na Mkemia Mkuu wa Serikali, Dk. Fidelis Mafumiko wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa bajeti na mwelekeo wa Mamlaka hiyo.

“Pia katika kuendelea kuboresha huduma zetu Taasisi imeruhusu biashara kubwa ya uingizaji wa kemikali nchini hususan Kemikali ya Salpha.

Akizungumzia kuhusu malalamiko ya mchakato wa kupata majibu ya vinasaba amesema  kawaida sampuli huwekwa maabara kwa siku 1 hadi 21 na inategemea sampuli ngapi zimepokelewa.

Dk. Mafumiko amesema sampuli hupitia katika hatua za kuchunguza, kukausha, kuchenjua, kuikuza na kukokotoa sampuli ambapo hatua zote zina muda wa saa ya kisayansi ambayo sio chini ya saa 12.

Aidha amesema vibali vya uingizaji wa kemikali nchini vimeongezeka kutoka 49,234 mwaka wa fedha 2020/21 hadi kufikia 63,588 katika mwaka wa fedha 2021/2022.

Amesema ni ongezeko hilo ni la vibali 14,354 ambalo limetokana na Serikali kuendelea kuboresha na kuweka mazingira wezeshi ya biashara ya kemikali nchini.

Aidha, amesema idadi ya wadau na shehena za mizigo ya kemikali zinazoingizwa nchini imeendelea kuongezeka.

Amesema katika kipindi cha mwaka 2021/2022 imefanikiwa kusajili wadau wanaojihusisha na shughuli za kemikali 1,087 ikilinganisha na wadau 1,057 waliosajiliwa kwa mwaka 2020/21 ikiwa ni ongezeko la wadau 30.

Dk. Mafumiko amesema mwaka 2021/22, Serikali imeiwezesha taasisi hiyo kununua mitambo na vifaa vya kisasa kwa ajili ya kuendelea kuboresha uchunguzi wa kisayansi wa kimaabara vyenye thamani ya Sh bilioni 22.

Amesema mitambo na vifaa hivi vilivyonunuliwa ni mitambo mikubwa mitatu na midogo 83 ambayo ni kwa ajili ya kuimarisha uchunguzi wa kimaabara.

Amesema  lengo la kuendelea kutoa huduma za uchunguzi wa kimaabaara kwa wananchi kwa haraka na kwa wakati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles