24.1 C
Dar es Salaam
Friday, April 26, 2024

Contact us: [email protected]

Mwakyembe: Hatupo tayari kuburuzwa na Kenya

Dr-Harrison-MwakyembeVeronica Romwald na Shamimu Mattaka, Dar es Salaam
SERIKALI ya Tanzania imesema haipo tayari kuburuzwa na Serikali ya Kenya kurekebisha mkataba wa mwaka 1985 unaotoa mwongozo wa ushirikiano katika sekta ya utalii kwa nchi hizo.
Kauli hiyo imekuja baada ya Kenya kuzuia magari ya kitalii yenye usajili wa Tanzania kuchukua na kushusha watalii katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyata (JKIA).
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, alisema Serikali haiwezi kurekebisha mkataba huo bila kujua namna ambavyo utaleta tija kwa taifa.
“Desemba 22, mwaka jana Kenya ilitoa amri ya kuzuia magari yenye usajili wa Tanzania kuchukua na kushusha wataalii wanaotumia uwanja wa JKIA wakiwa njiani kuja kutembelea vivutio vya utalii.
“Baada ya uamuzi huo, Januari 16, mwaka huu, Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, Lazaro Nyalandu, alifanya majadiliano na Waziri wa Masuala ya Utalii wa Kenya ili kutafuta ufumbuzi wa jambo hilo,” alisema.
Dk. Mwakyembe alisema mkataba umeelekeza maeneo mwafaka kwa ajili ya kubadilishana watalii ukizingatia kuwaondolea bughudha, hususan katika miji ya mipakani pamoja na miji rasmi iliyopendekezwa na kukubalika na pande zote mbili, ikiwamo Nairobi ambako ndipo ulipo uwanja wa JKIA.
“Kwa kuzingatia historia na uzito wa suala lenyewe, Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki iliona kuna umuhimu wa kuhusisha wizara nyingine zikiwamo Uchukuzi, Mambo ya Nje, Viwanda na Biashara, Fedha, Ulinzi, Mambo ya Ndani, Maliasili na Mazingira, pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi na Uongozi wa Sekta Binafsi ili kupata msimamo wa nchi wa pamoja kabla ya mkutano wa pamoja na Serikali ya Kenya,” alisema.
Alisema hata hivyo, kabla ya viongozi wa nchi hizo mbili kukutana, Waziri wa Masuala ya Afrika Mashariki, Biashara na Utalii wa Kenya, Phyllis Kandie, alimwandikia Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dk. Richard Sezibera na kumnakili Waziri Nyalandu kuhusu uamuzi wake wa kurejesha amri ya awali.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles