25 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

Mvuvi aliyesaidia uokoaji kuajiriwa jeshini

Na Mwandishi Wetu, Bukoba

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameagiza kijana Jackson Majaliwa, mvuvi wa Bukoba aliyefanikisha abiria 24 wa ndege ya Precision Air iliyopata ajali kuajiriwa kwenye Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

Hilo limesemwa leo Jumatatu, Novemba 7, 2022 na Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa wakati wa ibada maalum ya kitaifa ya kutoa heshima za mwisho kwa miili 19 waliofariki katika ajali hiyo iliyotokea jana Jumapili.

Majaliwa amesema pamoja na mambo mengine, kijana huyo atapewa mafunzo zaidi ya uokoaji na kujengewa ujasiri wa kushiriki shughuli mbalimbali za uokoaji.

“Rais Samia ameguswa na ujasiri wa kijana huyu na ameiagiza wizara ya mambo ya ndani kumwajiri katika Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kwa ajili ya mafunzo zaidi na kumjengea ujasiri.

“Nakuagiza waziri wa mambo ya ndani kutekeleza hilo haraka kwa kuchukua maelezo yote muhimu ya kijana huyu jasiri kwa hatua zingine,” amesema Majaliwa

Pamoja na kijana huyo, Majaliwa amesema Serikali inatambua juhudi na jitihada za wavuvi wengine waliosaidia uokoaji huku akiahidi taratibu zitafanyika kuwawezesha.

Kijana Majaliwa Jackson tayari amekabidhiwa zawadi ya Sh milioni 1 kama ishara ya kutambua juhudi na moyo wake wa kujitolea zilizotolewa na Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila.

Katika juhudi hizo, Majaliwa alijeruhiwa na mlango wa ndege na kukimbizwa hoaspitali ya rufaa mkoa wa Kagera kwa matibabu akiwa na majeruhi wengine 25 wa ajali hiyo wakiwemo abiria 24 na mfanyakazi wa uwanja wa ndege wa Bukoba aliyezimia kwa mshtuko.

Waziri Mkuu Majaliwa pia ametangaza kuwa Serikali itagharamia mazishi ya wote waliopoteza maisha katika ajali hiyo na kuwaagiza wakuu wa mikoa kusimamia suala hilo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles