26.6 C
Dar es Salaam
Sunday, October 1, 2023

Contact us: [email protected]

NMB yatoa elimu ya fedha kwa Chama cha Wakandarasi Wanawake Tanzania

Na Mwandishi Wetu

Benki ya NMB jana imetoa elimu kuhusu masuala ya fedha kwa mamia ya wakandarasi wanawake wa Kitanzania waliokutana jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wakandarasi wanawake lililoandaliwa na Chama cha Wakandarasi Wanawake Tanzania (TWCA).

Mkutano huo ulifadhiliwa na Benki ya NMB kwa shilingi milioni 10 ulifanyika chini ya kaulimbiu “Elimu ya fedha kwa maendeleo endelevu ya biashara na viwanda”

Akizungumza wakati wa kongamano hilo, Afisa Mkuu Huduma Shirikishi wa Benki ya NMB, Nenyuata Mejooli alisema benki hiyo imedhamiria kwa dhati kufanikisha ushirikishwaji wa kifedha nchini Tanzania na itaendelea kufanyia kazi azma hiyo kwa kusambaza huduma za kibenki kwa wafanyabiashara wasio na benki ikiwa ni pamoja na biashara zinazomilikiwa na wanawake, jamii na watu binafsi kote nchini kupitia mtandao wake mpana wa matawi zaidi ya 228, zaidi ya ATM 750 na mawakala wa benki 17,000.

“Mwaka 2020, benki yetu ilizindua jukwaa la wanawake yaani ‘NMB Jasiri’ lenye lengo la kuwapa wanawake suluhisho na huduma kama mikopo yenye vigezo nafuu, amana za uwekezaji na akiba kwa njia ya kidigitali, mafunzo, maonyesho na warsha kama hizi,” alisema.

Mejooli alisema kwa mwaka huu kupitia Jukwaa hilo hilo la NMB la NMB Jasiri, benki yake imepeleka neema kwa Wanawake Wakandarasi kwa njia ya mikopo na kuongeza kuwa tayari benki imetoa mikopo 30 kwa wanawake makandarasi yenye thamani ya Sh bilioni 1.8.

Mwenyekiti wa Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB), Mhandisi Consolata Ngimbwa wakati wa hafla hiyo alipongeza ushirikiano wa NMB na chama cha wanawake na kuwataka wakandarasi wanawake kuzingatia ufanisi wanapotekeleza majukumu yao.

“Fanyeni kazi kitaalamu mnapopata zabuni kwa kutumia watu wenye uwezo na wenye taaluma. Hi itasaidia makampuni yanayomilikiwa na wanawake kukua na kupiga hatua.

“Pia mnapaswa kuja na takwimu halisi katika zabuni zenu kwani kunukuu kiasi kidogo kunakuhakikishia zabuni tu lakini biashara yako haitakuwa uendelevu wa biashara,” alisisitiza.

Naye Rais wa TWCA, Judith Odunga wakati wa hafla hiyo aliitaka benki ya NMB kutafuta njia za kutoa mikopo kwa wakandarasi wanawake ili kuwawezesha kununua mitambo ya kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.

“Tunaiomba benki kutoa mikopo kwa wakandarasi wanawake ili kuwawezesha kukuza biashara zao na hii itawawezesha kushindana vyema.

Kwa sasa, kampuni nyingi za wanawake wakandarasi zipo kwenye daraja 6 na 7 na nia yetu nikuona kampuni hizo zikipiga hatua. Inapowezekana, benki inapaswa kukubali mitambo yao kama dhamana,” alisema.

Awali, mmoja wa mlezi wa chama hicho Getrude Mongella wakati wa hafla hiyo aliwataka wakandarasi wanawake kujituma zaidi na kubuni mbinu za kutafuta fursa za biashara zilizopo katika sekta ya ujenzi huku akisisitiza kuwa sekta hiyo ni miongoni mwa sekta zinazotengewa fedha kubwa katika bajeti ya serikali kila mwaka.

“Kuna fedha nyingi katika sekta ya ujenzi. Wanawake wanahitaji kuweka mikakati na kunyakua fursa katika sekta hiyo kikamilifu,” Mongella alisema.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Aisha Amour wakati wa hafla hiyo alisema tayari serikali imeweka mazingira mazuri ya biashara na sera za kuwezesha wanawake kushiriki kikamilifu katika sekta ya ujenzi.

Aliwataka wanawake kuunda ushirikiano na ubia kwenye kampuni za na kuongeza kuwa hii itasaidia kuboresha ufanisi wao na utoaji wa huduma.

“Makampuni ya wanawake lazima yaunde ubia kama yanataka kusindana kikamilifu kupata zabuni kubwa.

Nia ya Serikali ni kuona makampuni ya ndani yanakua na sisi kama serikali tunaendela kuboresha sera zitakazo boresha mazingira ya biashara,” alisisitiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,770FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles