23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

MVUTANO WAIBUKA UCHAGUZI SPIKA WA EALA

Na ABRAHAM GWANDU-ARUSHA


HALI ya sintofahamu imeibuka katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA), kuhusu namna atakavyopatikana Spika wa Bunge hilo.

Hatua hiyo imekuja huku mabishano makali yameibuka kuwa ni nchi gani inatakiwa kutoa Spika kutokana na utaratibu waliojiwekea nchi wanachama.

Hayo yaliibuka jana mjini Arusha baada ya Katibu wa Bunge la EALA, Kenneth Matede, kusoma arodha ya wagombea wa uspika na kuwapo jina la Adam Kimbisa kutoka Tanzania.

Mbali na Kimbisa, wagombea wengine ni Martine Ngoga kutoka Rwanda na Leontine Nzeymana wa Burundi.

Baada ya kutajwa kwa jina la Kimbisa, yaliibuka malumbano makali kutoka miongoni mwa wabunge, huku wengine wakisema kuwa Tanzania haikutakiwa kuwa na mgombea kutokana na utaratibu waliojiwekea wa Spika kupatikana kwa mzunguko kwa nchi wanachama.

Hoja hiyo ilizua mtafaruku huku wabunge wa Tanzania na Burundi wakilazimika kutoka nje kupinga, wakiweka msimamo kwamba Spika hatakiwi kuchaguliwa kwa kufuata mzunguko.

Hadi sasa nchi wanachama ambao wameshatoa Spika wa Bunge tangu lilipozinduliwa tena mwaka 2000, ni Tanzania, Kenya na Uganda. Safari hii anatakiwa kutoka Rwanda au Sudan Kusini.

Katika uchaguzi huo, mgombea Martine Ngoga wa Rwanda, alionekana kuwa na ushawishi dhidi ya wagombea wengine waliotajwa katika kinyang’anyiro hicho.

Hata wabunge wa Tanzania waliporejea ukumbini, hawakubadili msimamo wao na hawakuwa tayari kueleza hasa ni kwanini wameamua kuwa na mgombea katika uchaguzi huo.

Kutokana na hali hiyo waliendelea kushikilia msimamo kuwa suala la zamu halina ulazima wowote kwa sababu idadi ya nchi wanachama imeongezeka kutoka tatu za awali hadi sita.

Kikao hicho cha Bunge kiliahirishwa hadi leo.

Akionekana kushangazwa na msimamo huo wa wabunge wa Tanzania, Mbunge Adam Mohamed Noor wa Kenya, alisema kitendo hicho kinapuuza busara zilizotumiwa na waasisi walioweka kanuni hiyo.

“Hili ni jambo dogo sana katika alama za utawala wa sheria na demokrasia, kama makubaliano yalikuwa kufuata zamu, kwanini Tanzania inashindwa kuheshimu hilo? Sisi wengine tunashangaa sana na hatuwezi kukubali mambo madogo namna hii yatishie kuvunja jumuiya yetu,” alisema Noor.

Kwa upande wake Mukassa Mbinde kutoka Uganda, alisema ni jambo lisilowezekana kwa Tanzania kuwasilisha jina la mgombea wa nafasi ya Spika katika Bunge hili kwani si zamu yao.

“Katika eneo hili, Tanzania ndio mfano wa kuigwa katika masuala ya utawala na demokrasia, hii nchi ni kubwa mno kuliko jambo dogo kama hili la kumpata Spika. Maeneo mengine yote iwe Katibu Mkuu wa Jumuiya, Jaji Mkuu na viongozi wa asasi zote zinazohusu eneo hili, tunawapata kwa zamu,” alisema Mbinde.

Kwa upande wao wabunge wote wa Tanzania hawakuwa tayari kuzungumzia msimamo wao huo, huku Kimbisa aliahidi kulizungumzia suala hilo leo kabla ya kikao cha Bunge ambacho kinatarajiwa kuanza saa nane mchana.

 

CHADEMA WATOA TAMKO

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetoa tamko na kusema kuwa pamoja na mambo mengine, ilitarajiwa kufanyika kwa uchaguzi wa Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles