28.6 C
Dar es Salaam
Monday, December 9, 2024

Contact us: [email protected]

MUZIKI WA DANSI UKIFA MASHABIKI WAKE MTAWAPELEKA WAPI?

ENDAPO ningembiwa kitu gani nikibadilishe kwenye tasnia ya muziki nchini basi ningebadilisha upepo wa Bongo Fleva uende sawa na muziki wa Dansi, muziki mama uliozaa aina zote za miziki unazozisikililiza.

Miaka ya 80 wakati haijulikana kama kuna muziki utazaliwa unaoitwa Bongo Fleva, muziki wa Dansi ulikamata sehemu kubwa ya jamii, vijana wa zamani mpaka wazee wa wakati huo waliuhusudu muziki huu.

Hakukuwa na lugha chafu zinazoweza kuvuruga maadili ya jamii yetu, hakukua na video zinazoonyesha sehemu kubwa ya miili ya wanawake ikiwa wazi ndiyo maana jumbe zilizosokotwa kwenye nyimbo zile zilifika mubashara kwa watu wote.

Sasa leo hii Bongo Fleva imetawala, muziki wa Dansi umeminywa na vyombo vya habari vimeutenga muziki huu, nauliza hivi ikitokea Dansi ikafa kabisa mamilioni ya mashabiki wake mtawapeleka wapi?

Ni kweli Dansi ya zamani na ya sasa imekuwa tofauti, wanamuziki wa zamani waliimba kulingana na mazingira ya wakati ule hata hawa wanamuziki wa sasa wanapiga muziki kulingana na mazingira ya sasa lakini hawapati nafasi ya kusikika sababu Bongo Fleva imepewa kipaombele.

Nafurahi kuona Sikinde Ngoma ya Ukae wanajaribu kukimbizana na wakati. Akina Mjusi Shemboza wanakung’uta gitaa kwa uhodari ili kukishawishi kizazi hiki cha dotcom kielewe muziki ni nini.

Maisha ya msanii wa Bongo Fleva na mwanamuziki wa Dansi yana utofauti mkubwa. Bongo Feva imewekwa kibiashara hivyo ni lazima vijana hawa watengeneze fedha ila upande wa muziki wa Dansi ni tofauti.

Dansi ni muziki wenye mashabiki wengi ila tatizo bado wadau hawajauweka katika levo za kibiashara ndiyo maana wanamuziki wake hawanufaiki kama wale wana Bongo Fleva.

Hivi sasa wasanii wa Bongo Fleva wanauza kazi zao kimtandao na kupata diliza matangazo kwenye kampuni mbalimbali lakini wanamuziki wa Dansi hutegemea maonyesho pekee.

Kuna ulazima madereva wanao iendesha Bongo Fleva wakaushika pia usukani wa muziki wa Dansi ili mambo yawe sawa kwa wanamuziki wote

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles