27.1 C
Dar es Salaam
Thursday, January 2, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Muswada wa habari kuwasilishwa bungeni

Na Debora Sanja, Dodoma
HATIMAYE Muswada wa Sheria ya kupata Habari na Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari ya Mwaka 2015, inatarajiwa kuwasilishwa bungeni katika mkutano wa 19 wa Bunge unaoanza leo mjini hapa.
Miswada hiyo inatarajiwa kuwasilishwa kwa hati ya dharura na inakusudiwa kupitishwa na Bunge katika hatua zake zote.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa mjini hapa jan,a mbali na miswada hiyo kuwasilishwa, pia miswada mingine minne inatarajiwa kuwasilishwa kwa hati ya dharura.
“Miswada hiyo ni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ushindani wa mwaka 2015,Muswada wa Sheria ya makosa ya Mtandao wa mwaka 2015,Muswada wa Sheria ya Miamala ya Kielektroniki wa mwaka 2014 na Muswada wa Sheria ya Gesi Asilia wa mwaka 2015,”ilieleza taarifa hiyo.
Taarifa hiyo hiyo inaeleza kuwa miswada mingine 15 itasomwa kwa mara ya pili bungeni na kupitishwa na Bunge katika hatua zake zote kwa mujibu wa kanuni ya 86(1) ya kanuni za Bunge .
Miswada hiyo ni ule wa Sheria ya Udhibiti wa Ajira za Wageni wa mwaka 2014, Muswada wa Sheria ya Mifumo ya Malipo ya Taifa wa mwaka 2015, Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Kodi mwaka 2014 na Muswada wa Sheria ya Takwimu wa mwaka 2014.
Mingine ni Muswada wa Sheria ya Tume ya Kudhibiti Ukimwi wa mwaka 2014, Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa mwaka 2014, Muswada we Sheria ya Udhibiti na Usimamizi wa Dawa za Kulevya wa mwaka 2014 na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Stakabadhi Ghalani.
“Miswada mingine itakayowasilishwa ni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Uhamiaji wa mwaka 2014, Muswada wa Sheria ya Kudhibiti Silaha wa mwaka 2014, Muswada wa Sheria ya Wataalamu wa Kemia wa mwaka 2014 na Muswada wa Sheria ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali wa mwaka 2014.
“Mingine ni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa mwaka 2014, Muswada wa Sheria ya Bajeti wa mwaka 2014 na Muswada wa Sheria ya Baraza la Vijana wa mwaka 2015,” ilieleza taarifa hiyo.
Mbali na miswada hiyo pia Bunge hilo litaridhia Azimio la Makubaliano ya Msingi ya Ushirikiano Katika Bonde la Mto Nile.
Katika Mkutano 19 pia maswali 170 yanatarajiwa kuulizwa, 18 yakiwa kwa Waziri Mkuu.
Ratiba ya  shughuli zitakavyowasilishwa itatolewa baada Kamati ya Uongozi kukutana kuanzia leo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles