27.9 C
Dar es Salaam
Monday, June 24, 2024

Contact us: [email protected]

Muswada Bima ya Afya kwa Wote kuingia bungeni Septemba

Na ARODIA PETER

DODOMA

SERIKALI iko mbioni kukamilisha muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa wote na kuuwasilisha bungeni Septemba.

Pia wizara hiyo ipo katika maandalizi ya muswada wa marekebisho ya Sheria ya VVU na Ukimwi sura Na 431 ili kuruhusu watu kujipima wenyewe na kushusha umri wa mtu kupima bila ridhaa ya mzazi au mlezi kutoka miaka 18 hadi 15. 

Waziri wa  Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, akisoma bajeti ya wizara yake kwa mwaka 2019/20 bungeni jana, alisema maandalizi ya mpango huo yamekamilika ikiwamo mkutano wa kuelimisha wabunge kuhusu mkakati wa uboreshaji mfumo wa ugharamiaji wa bima  za afya.

Katika maandalizi hayo, alisema wabunge 19 walifanya ziara nchini Rwanda na Ghana Disemba mwaka jana kwa lengo la kupata uzoefu wa namna nchi hizo zilivyoweza kutekeleza mfumo huo wa bima kwa wote.

Katika hotuba hiyo, waziri Ummy alitaja vipaumbele vya wizara hiyo kwa mwaka 2019/20 kuwa ni pamoja na kuendelea kununua na kusambaza chanjo kulingana na mahitaji, kuwakinga watoto wa umri chini ya mwaka mmoja na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ambapo Sh bilioni 30 zimetengwa.

“Wizara itaendelea kutekeleza afua mbalimbali za huduma ya kinga ikiwa ni pamoja na kupunguza vifo vya kina mama vitokanavyo na uzazi na vifo vya watoto.

“Kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza kama vile kisukari, moyo, shinikizo la damu, saratani na magonjwa sugu kama vile pumu.

Kuhusu ukimwi, Ummy alisema huduma za tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na maambukizi na VVU zimeendelea kutolewa na idadi ya watu wanaotumia dawa ya kupunguza makali ya virusi vya Ukimwi imeongezeka kufikia wati 1,103,016 mwa Machi.

Alisema pia wizara yale kwa kushirikiana ile ya Viwanda na Biashara na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) na Bohari ya Dawa imeandaa mwongozo unaoainisha fursa mbalimbali za uwekezaji katika viwanda vya dawa na vifaa tiba.

Mwongozo huo utarahisisha upatikanaji wa taarifa katika uwekezaji wa viwanda vya dawa nchini ambapo hadi kufikia Machi mwaka huu viwanda nane vya dawa vinaendelea kujengwa nchini.

Aidha Ummy alisema wizara yake imeendelea kuimarisha huduma za matibabu ya kibingwa kuokoa maisha ya wananchi wengine kupunguza idadi ya wagonjwa wanaopewa rufaa ya matibabu nje ya nchi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
588,000SubscribersSubscribe

Latest Articles