25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

MUSUKUMA AZUA JAMBO BUNGENI

Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA

MBUNGE wa Geita Vijijini (CCM), Joseph Musukuma jana alichafua hali ya hewa bungeni baada ya kudai kuwa  ni wabunge wawili au watatu tu ndani ya bunge ndio hawajapita kwa waganga wa kienyeji kuingia bungeni.

Baada ya kauli hiyo, wabunge walionekana wakipingana naye huku wengine wakiomba utaratibu kwa Spika na wengine walisikika wakitamka kuwa awaombe radhi.

Hata hivyo Naibu Spika Dk.Tulia Ackson hakutoa nafasi kwa mbunge yeyote.

Musukuma alizua tafrani hiyo wakati akiuliza swali la nyongeza. 

Katika swali lake, Musukuma alisema kumekuwapo na kauli kuwa wasanii wanatumika wakati wa uchaguzi na wanasiasa lakini zikiisha hawasaidiwi.

Alisema jambo la kushangaza hata Wabunge nao wamekuwa wakiwatumia waganga wa kienyeji lakini uchaguzi ukiisha wanawaletekeza.

“Kwa karama niliyonayo nikiangalia humu ndani wakati wa uchaguzi wawili au watatu hamkupita kwao akiwemo Mzee Selasini (Joseph Mbunge wa Rombo-Chadema)

“Si hao tu wabunge peke yake bali jamii nzima na waganga hawa baada ya uchaguzi tunawatekeleza na kuwatumia polisi, je serikali haioni umuhimu wa kujenga chuo cha kuwasaidia waganga hawa hata kama ni kwa elimu ndogo’’aliuliza Musukuma huku 

wabunge wakiangua kicheko.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, alisema waganga wa jadi wamekuwa na mchango mkubwa na serikali inalitambua hilo na itaendelea kuwaboreshea huduma zao ikiwamo kuweka mawakala wilayani ambao wanafanya kazi ya kuwatambua na kuwasajili.

Katika swali la msingi, Mbunge wa Ushetu, Eliasi Kwandikwa (CCM) alitaka kujua ni waganga wangapi wa kienyeji walikamatwa katika halmashauri ya Wilaya ya Ushetu na wangapi walifikishwa mahakamani na kutiwa hatiani katika kipindi hicho.

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusufu Masauni aliwataja waganga waliokamatwa wilayani Ushetu kuwa ni 26 na kushitakiwa kwa makosa mbalimbali ikiwemo kufanya uganga bila ya kibali na kupatikana kwa nyaraka za serikali.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles