23.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 24, 2024

Contact us: [email protected]

WAJUE MABILIONEA 10 WAPYA WANAOWIKA TANZANIA

 

Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM

IDADI ya mamilionea wa Tanzania kwa mujibu wa Jarida la Forbes inaendelea kuongezeka wakati taifa hilo liking’ara kiuchumi kulinganisha na mataifa mengine ya Afrika Mashariki.

Mbali ya majina yaliyozoeleka ya mabilionea kama vile Mohammed Dewji, Rostam Azizi na Said Salim Bakhresa, kuna wengine wanaojulikana kidogo.

Majina yao hayasikiki barani Afrika na kuna wanaofahamika kidogo hata katika taifa hilo, lakini ni wafanyabiashara waliofanikiwa nchini Tanzania.

Wafuatao kwa mujibu wa Forbes ni wafanyabiashara mamilionea 10, ambao wanamiliki biashara zinazoingiza kipato cha Dola za Marekani milioni 50 au zaidi kwa mwaka.

 Ally Awadh

Mfanyabiashara wa mafuta nchini Tanzanian, Ally Edha Awadh ni mwasisi na Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Kampuni ya Lake Oil Group, moja ya himaya za kibiashara za sekta ya mafuta na uchukuzi zinazokua kwa kasi Afrika Mashariki.

Awadh alianzisha kampuni hiyo mwaka 2006 akiwa na umri wa miaka 26, wakati alipopokea moja ya vibali adimu vinavyotafutwa zaidi kutoka Serikali ya Tanzania kuingiza na kuuza bidhaa za petroli katika soko la ndani.

Shekhar Kanabar

Mfanyabiashara Shekhar Kanabar (35), ni CEO wa Himaya ya Kampuni za Synarge, yenye umri wa miaka 50 ikianzia kwa umiliki wa familia nchini Tanzania na imejikita mizizi katika sekta ya uzalishaji, uhuishaji wa betri na vipuri vya magari.

Baba wa Kanabar alianzisha biashara katika miaka ya 1960 zikijihusisha na nguo, lakini zimekua tangu hapo na kuhusisha kampuni mbalimbali zenye waajiriwa zaidi ya 150 na mapato ya mamilioni ya dola.

Subash Patel

Mwaka 1992, Subash Patel alianza kujihusisha na biashara ya mashine mbalimbali jijini Dar Es Salaam. Katika kipindi cha miongo miwili, ameigeuza biashara hiyo katika Motisun Group, himaya ya kampuni tofauti 15 katika seta za chuma, madini, plastiki, rangi, usindikaji vyakula na mali zisizohamishika. Na hoteli za kitalii ikiwamo Sea Cliff Resort ya Zanzibar na Hotel White Sands  Dar es Salaam.

Ghalib Said Mohamed

Milionea Ghalib Said Mohamed alianzia kwa kufanya kazi katika biashara za baba yake katika kilimo cha korosho na biashara nyinginezo kwa ujumla.

Haikuchukua muda akaondoka na kuanzisha kampuni yake ya GSM Group, himaya ya kampuni inayojihusisha na biashara mbalimbali kama vile uchukuzi, lojistiki, vyombo vya habari, uzalishaji, mali zisizohamishika na huduma za kifedha na rejareja.

Fida Hussein Rashid

Mwaka 1973 Fida Hussein Rashid alianzisha Kampuni ya Africarriers Group, mwasisi wa biashara ya magari mitumba nchini Tanzania. Africarriers ikaondokea kuwa moja ya kampuni za kwanza Afrika Masharkiki kuingiza magari ya Kijapan kama vile Toyota katika ukanda huo. Kampuni hiyo kwa sasa ni msambazaji muhimu wa magari chapa Eicher and Golden Dragon.

Salim Turky

Salim Turky ni Mbunge wa Mpendae (CCM) ni mmoja wa wafanyabiashara waliofanikiwa zaidi Tanzania.

Himaya yake ya Kampuni za Turkys, ambayo aliianzisha katika miaka ya 1980 inajishughulisha katika uzalishaji wa saruji, hoteli, hospitali na huduma za mawasiliano.

Yogesh Manek

Manek alianzisha himaya ya Kampuni za MAC nchini Tanzania katika miaka ya 1980. Biashara yake maarufu zaidi ni Benki ya EXIM, moja ya benki kubwa tatu nchini Tanzania linapokuja suala la wingi wa wateja na mali. Pia ni mmiliki wa Kampuni ya Bima ya Heritage na Strategis, taasisi inayoongoza ya afya nchini (HMO).

Abdulaziz Abood

Mwingine ni Mbunge wa Morogoro Mjini, Abdulaziz Abood (CCM), ambaye pia mwanasiasa na mwanzilishi wa Abood Group, himaya ya kibiashara inayojishughulisha na kila kitu kuanzia usafirisaji wa abiria, usambazaji wa petroli, vyombo vya habari hadi uwindaji wa kitalii.

Yusuf Manji

Manji alirithi kampuni ndogo ya biashara kutoka kwa wazazi wake na kuigeuza kuwa Quality Group, himaya ya kampuni zilizojikita katika utoaji wa huduma za kifedha, huduma za afya, usindikaji chakula na mali zisizohamishika. Manji pia ni mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, ambayo bila ubishi inatajwa kuwa klabu ya mpira wa miguu iliyofanikiwa zaidi Tanzania.

 Haroon Zakaria

Murzah Oils, kampuni ambayo Haroon Zakaria aliianzisha mwaka 1997, ni moja ya kampuni zinazoongoza Afrika Mashariki kwa uzalishaji wa mafuta ya kura, maliwato na sabuni za kufulia, mafuta ya kula kutokana na mimea, siagi za mikate na margarine.

Kampuni ina rekodi ya mapato ya dola milioni 100 kwa mwaka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles