30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

MUSEVENI KUWANIA URAIS MUHULA WA SITA

KAMPALA, UGANDA

MAHAKAMA ya Katiba nchini Uganda imemruhusu rais wa nchi hiyo, Yoweri Kaguta Museveni, mwenye umri wa miaka 73, kuwania muhula wa sita wa urais katika uchaguzi uliopangwa kufanyika mwaka 2021.

Mnamo Januri mwaka huu, Rais Museveni, ambaye amekuwa madarakani kwa miaka 31, aliidhinisha sheria inayofuta ukomo kwa mgombea mwenye umri wa miaka 75 kuwania katika uchaguzi wa urais, na hivyo kusababisha maandamano upande wa upinzani, ambao ulishutumu mbinu za kutaka kukaa madarakani milele.

Baada ya hatua hiyo, muungano wa vyama vya upinzani uliwasilisha malalamiko yao mahakamani. Hata hivyo, malalamiko hayo hayakufanikiwa hadi sasa.

Idadi kubwa ya Majaji wa Mahakama ya Katiba waliokutana katika kikao maalumu huko mjini Mbale, takribani kilomita 225 mashariki mwa jiji la Kampala, waliamua kupitisha sheria hiyo inayofuta ukomo kwa wagombea wenye umri wa miaka 75 kuwania urais.

Sheria iliyopitishwa na Majaji hao inafuta ile ya awali iliyoidhinishwa na Rais Museveni ya kuweka ukomo umri. Hatua hiyo inaungana na nyingine ya mwaka 2005, ambayo iliondoa ukomo wa mihula ya urais.

Museveni, ambaye alichukua hatamu ya uongozi wa nchi mwaka 1986, akiwa mkuu wa jeshi la waasi, aliwahi kusema kuwa, viongozi ambao wanakaa muda mrefu madarakani wanakuza chuki na kusababisha matatizo barani Afrika.

Lakini wakati alipokuwa mgombea urais kwa muhula wa tano mwaka wa 2016, alisema muda haujafika yeye kuachia ngazi, akisema bado ana kazi nyingi za kufanya

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles