27.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

SHABIKI SIMBA ASHINDA MILIONI 126.2 ZA M-BET

Na MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM

SHABIKI wa timu ya Simba na Barcelona ya Hispania, Ali Ahmad Fundi (40), ameshinda Sh 126,241,620, baada ya kubashiri kwa usahihi mchezo wa Perfect 12 wa Kampuni ya M-Bet.

Fundi, ambaye ni mkazi wa Lindi, alisema kuwa, alibashiriki kwa kupitia simu yake ya mkononi na kuibuka na kufanikiwa kushinda kiasi kikubwa hicho cha fedha.

“Nimefarijika sana, sikuamini, kwani awali marafiki zangu walisema napoteza fedha, lakini niliendelea kucheza baada ya kuona baadhi ya Watanzania wanashinda fedha nyingi kupitia mchezo wa Perfect 12, niliamini siku moja nami nitakuwa mmoja wa washindi,” alisema Fundi.

Alisema kuwa ametumia Sh 1,000 tu na kuibuka na kitita kikubwa cha fedha. “Kabla ya kushinda, nilibet mara tatu na kutumia Sh 3,000, sikukata tamaa na leo kuibuka na ushindi,” alisema Fundi.

Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi, alisema kuwa, kupitia ushindi huo, serikali ilijipatia Sh 25,248,124, ikiwa kodi ya asilimia 20 kwa mujibu wa sheria.

Mushi alisema kuwa, mbali ya Fundi, pia kulikuwa na washindi 1,058 walioshinda kwa kubashiri kwa usahihi mechi tisa, ambao walizawadiwa Sh 1,854,630, huku washindi watu 175 waliweza kubashiri kwa usahihi mechi 10 na kuzawadiwa Sh 2,472,840 na watu 11 waliweza kubashiri michezo 11 kwa usahihi na kuzawadiwa Sh 2,884,980.

“Kwa droo ya 840 pekee, tumeweza kutoa washindi 1,243 na kutumia fedha Sh 133,464,070 kuwazawadia washindi. Tunaomba  Watanzania kuendelea kubeti kwa kutumia michezo yetu na kufaidika kwa kuondoa umaskini,” alisema Mushi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,327FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles