25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Muleba yakamilisha ujenzi wa vyumba vya madarasa

Renatha Kipaka, Muleba

Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Muleba mkoani Kagera, Elias Kayandabila amekabidhi vyumba 234 vya madarasa kwa Mkuu wa wilaya ya Muleba, Toba Nguvila, tukio ambalo limefanyika katika shule ya sekondari ya Anna Tibaijuka.

Akizungumza jana wakati wa kukabidhi vyumba hivyo, shule ya sekondari ya Anna Tibaijuka ambayo ilikuwa na ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa, Elias Kayandabila ametoa pongezi kwa wasaidizi wake kuanzia ngazi ya wilaya hadi ngazi za kata ambazo zilipokea fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba hivyo.

Amesema kazi iliyofanyika ni kubwa na nzuri ambayo wameifanya na kuonyesha kufurahishwa na ushirikiano uliokuwepo baina ya wabunge, Chama Cha Mapinduzi(CCM) na Watumishi wote wa Halmashauri.

“Haikuwa kazi rahisi, binafsi nawapongeza sana watumishi wenzangu, wasaidizi wangu na walimu wote ambao mmejitoa kwa kila namna kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati, tusichoke katika kutimiza majukumu yetu kwa jamii inayotutegemea”, amesema Kayandabila.

Hata hivyo, akipokea madarasa hayo Mkuu wa Wilaya ya Muleba amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa utoaji wa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba hivyo ambao kwa kiasi kikubwa umesaidia kupunguza adha ya kuwachangisha wananchi kwa ajili ya ujenzi wa vyumba hivyo.

“Tuwe wakweli wilaya ya Muleba zisingekuwa fedha hizi kutolewa kwa ajili ya ujenzi wa vyumba hivi mwezi wa Januari tungepata tabu lakini kwa sasa watoto wanaenda kukaa kwenye vyumba vya madarasa vilivyokamilika na kwa idadi inayokubalika kwa maana kila darasa sasa litakuwa na uwezo wa kuwa na idadi ya wanafunzi 45-50,” amesema Nguvila.

Pia ametoa pongezi za dhati kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba, Elias Kayandabila pamoja na Wabunge, Madiwani, Watendaji, Wakuu wa shule na Wataalamu katika Idara za Elimu, ujenzi na manunuzi kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kusimamia ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa hadi kukamilika.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Muleba, Magongo Justus, ameishukuru ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji pamoja na wataalamu wake kwa namna ambavyo wameshirikiana kwa pamoja kuhakikisha kazi inakamilika kwa muda lakini pia amemshukuru mkuu wa wilaya ya Muleba kwa maelekezo yake na ufuatiliaji wa karibu kuhakikisha kwamba kazi inakamilika kwa wakati.

Kwa upande wao Wabunge wa Jimbo la Muleba Kusini na Muleba Kaskazini Dk. Oscar Kikoyo na Charles Mwijage wametoa pongezi kwa Rais Samia pamoja na uongozi wa Halmashauri kwa kuhakikisha wanasimamia kazi ya ujenzi kumalizika kwa wakati na kutoa wito kwa wazazi kuwapeleka watoto wao shule kwani tayari vyumba vya madarasa vimekamilika.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles