27.7 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 21, 2024

Contact us: [email protected]

Muigizaji Mzee Jengua afariki dunia

Na Jeremia Ernest, Dar es Salaam

Muigizaji mkongwe kwenye tasni ya filamu nchini, Muhammed Fungafunga ‘Jengua’ amefariki dunia leo Jumanne Desemba 15, 2020 nyumbani kwa mtoto wake Mkuranga mkoani Pwani.

Enzi za uhai wake Fungafunga alijizolea umaarufu wa kuvaa uhusika wa ukali na uchawi mpaka kupelekea kuogopwa katika jamii.

Mbali ya kuwa kuigiza marehemu Mzee Jengua alikuwa na kipaji cha kuchezea nyoka, alikuwa akifanya maonesho sehemu mbalimbali, pia ni mfugaji wa kuku.

Katika mahojiano yake na nyimbo vya habari aliwahi kusema jambo ambalo hawez kusahau katika maisha yake aliwahi kurogwa akazimia kwa muda wa siku nne.

“Nakumbuka nilikuwa sehemu moja Mang’ola (Morogoro) nashuti filamu mimi kama mchawi, nimemuibua mtu kwenye bwawa halafu nikaruka naye juu na kupotea naye.

“Baada ya kufunguka kipengele kingine ikaonekana kwamba nipo naye nyumbani ni ndondocha, sasa ‘maedita’ wakawa ‘wameediti’ hicho kipande walikuwa na kawaida ya kuweka TV nje usiku halafu wanaonesha vile vipande tulivyoshuti, basi nimelala asubuhi kuamka nikapigwa kitu (kurogwa), nikazimia siku nne, baadaye mke wangu alipokuja nilipelekwa hospitalini nikachomwa sindano 16 na dripu sita, lakini sikuzinduka, mpaka mzee Msisiri (naye mwigizaji) akanitanifutia shekhe akanifanyia dua, ndiyo nikazinduka,” alinukuwa Mzee Fungafunga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles