27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Muhongo: Mitambo ya kuzalisha umeme ina matatizo

hongoNA RACHEL MRISHO, DODOMA

SERIKALI imekiri kuwapo kwa tatizo katika mitambo na kusababisha ukatikaji wa umeme katika maeneo mbalimbali.

Kauli hiyo ilitolewa bungeni jana na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa  Sospeter Muhongo, wakati akijibu swali la msingi lililoulizwa na Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Vedasto Ngombale (CUF), aliyehoji nini kiini cha umeme unaozalishwa kutokana na gesi ya Songosongo kukatika mara kwa mara.

Alisema Serikali imebaini kuwa mitambo mingi hufanya kazi kwa muda wa miaka miwili tu na kuanza kuleta usumbufu.

Awali, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk. Medard Kilemani, alijibu kwamba mtambo mmoja wa umeme unaofuliwa kutoka Somanga Fungu unaotumika katika wilaya za Kibiti na Rufiji haufanyi kazi.

Alisema ukatikaji huo wa umeme unatokana na hitilafu katika mitambo ya kuzalisha umeme na kusambaza umeme.

Baada ya majibu hayo, Profesa Muhongo alilazimika kusimama na kusema: “Naomba nilieleze Bunge ukweli Lindi na Mtwara kuna tatizo la umeme, Tanesco inafanya marekebisho mwisho wa mwaka huu tatizo litakamilika.

“Si mitambo ya Somanga Fungu pekee ndiyo ina matatizo, niwe mkweli kabisa maana kusema ukweli kuna faida, lipo tatizo kubwa mitambo yetu ikianza kufanya kazi ndani ya miaka miwili inakuwa na matatizo.

“Lazima tuwe wakweli mitambo ikiwamo Nyakato na Ubungo yote ina matatizo na kuhusu mitambo ya Songa Fungu aliyetengeneza mitambo si yule anayerekebisha tunachokifanya ni kuhakikisha mikoa ya Kusini inaingizwa katika gridi ya Taifa.”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles