21.1 C
Dar es Salaam
Saturday, August 13, 2022

Gondwe apiga marufuku usafirishaji madini

godwin-gondweNa Mwandishi Wetu, Tanga

MKUU wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, amepiga marufuku usafirishaji wa madini usiku badala yake ametaka yasafirishwe mchana.

Agizo hilo amelitoa mjini hapa jana baada ya kukamatwa kwa malori saba yakiwa yamebeba madini aina chuma na dolomati yakiwa yanatokea Kata ya Mgambo kuelekea mkoani Mtwara katika Kiwanda cha Dangote.

Gondwe alisema wafanyabiashara wengi wamekuwa wakisafirisha biashara hiyo usiku kwa lengo la kukwepa kodi na kuikosesha Handeni mapato.

“Tulipokamata magari hayo cha kwanza tuliwauliza kama wamelipa kodi na kama wamelipa kodi watuonyeshe makaratasi yanaonyesha kuwa wamelipa kodi,” alisema Gondwe.

Pia alisema madini yanaposafirishwa nje ya wilaya mfanyabiashara anatakiwa kuilipa Serikali Kuu asilimia tatu na halmashauri inatakiwa ilipwe asilimia 0.3 ya mauzo ya biashara hiyo ya madini.

Alisema wao kama halmashauri wanataka kila mfanyabiashara alipe kodi ili kuweza kuinua uchumi wa wananchi wa Handeni na Mkoa wa Tanga kwa ujumla.

Alisema Rais Dk. John Magufuli anataka  kuona wanaongeza mapato katika  halmshauri zao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Handeni, William Makufwe, alisema wamekuwa wakipoteza mapato kupitia wafanyabiashara wanaokwepa na kusababisha halmashauri kukosa mapato kwa kiasi kikubwa.

Kwa  Upande wake, Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Wilaya ya Handeni na Kilindi, Charles Kamuhanda, alisema kumekuwa na changamoto kubwa ya ulipaji wa kodi  kutoka kwa wafanyabiashara wa madini.

Kamuhanda alisema kati ya kampuni 37 zilizosajiliwa na ofisi ya madini wilaya na kulipa mrabaha ni kampuni mbili tu zinazolipa kodi kisheria na 35 hawalipi  jambo ambalo ni changamoto kubwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
198,592FollowersFollow
550,000SubscribersSubscribe

Latest Articles