Na.Shomari Binda, Musoma
MBUNGE wa Musoma vijijini,Profesa Sospeter Muhongo, amechangia mifuko 200 ya saruji katika ujenzi wa zahanati ya Kitongoji cha Kwikonero Kata ya Suguti mkoani Mara.
Ujenzi wa zahanati hiyo ni moja ya zahanati 16 zinazoendelea kujengwa kwenye jimbo la Musoma vijijini kupitia nguvu za wananchi, Serikali, wadau na mbunge wa jimbo hilo.
Akizungumzia ujenzi wa zahanati hiyo, Katibu wa mbunge, Hamisa Gamba, amesema jitihada kubwa zimekuwa zikifanyika katika sekta ya afya kwa kuwa ni muhimu.
Amesema bila kuwa na afya njema shughuli za kiuchumi haziwezi kufanyika ili wananchi wajipatie kipato na kuendeleza familia zao ikiwemo kuwapatia watoto elimu.
Hamisa amesema licha ya mbunge wa jimbo la Musoma vijijini kuchangi zahanati hiyo ya Kwikonero lakini pia amekuwa akichangia kwenye maeneo mengine ya ujenzi wa zahanati.
“Ujenzi wa zahanati ni juhudi za wananchi na serikali katika kuona juhudi hizo imechangia mifuko 50 ya saruji kuunga mkono na mbunge pamoja na wadau nao wamekuwa wakichangia.
“Sisi kama wasaidizi wa mbunge tunafatilia kuhakikisha ujenzi unaendelea vizuri kwenye maeneo yote ya ujenzi na kukamilika ili wananchi wapate huduma,”amesema Hamisa.
Ameongeza kuwa utaratibu ulishawekwa ndani ya jimbo kila zilipo juhudi za wananchi za ujenzi wa huduma za kijamii mbunge anachangi.a