25.5 C
Dar es Salaam
Friday, September 29, 2023

Contact us: [email protected]

Burudani kibao kupamba Usiku wa Ruvu Shooting

Na WINFRIDA MTOI, Mtanzania Digital

BAADA ya Simba na Yanga kutumia matamasha yao kutambulisha wachezaji, Ruvu Shooting nayo imekuja na la kwao na kulipa jina la Usiku wa Ruvu Shooting litakalofanyika Jumamosi Septemba 25,2021 Mlandizi, Pwani.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 21, Ofisa Habari wa Klabu ya Ruvu Shooting, Masau Bwire, amesema siku hiyo kutakuwa na burudani mbalimbali, mechi ya kirafiki, utambulisho wa jezi na wachezaji watakaounda kikosi cha msimu wa 2021/2022.

Amesema pia kutakuwa na wageni waalikwa ikiwamo viongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Aboubakar Kunenge.

Amewataja wasanii watakaotumbuiza siku hiyo kuwa ni Aslay, Dully Sykes, Dulla Makabila, Nick Mbishi Tunda Man na bendi ya Ruvu JKT.

“Kama ambavyo wamekuwa wakifanya hawa wakubwa wawili, Simba kuwa na Simba Day na Yanga Siku ya Wananchi, tutapita mule mule ila kuna utofauti kidogo, sisi tunasema siku wa Ruvu Shooting.

Kikosi cha Ruvu Shooting msimu uliopita

“Siku ya tarehe 25 ya mwezi huu kabla ya Usiku wa Ruvu Shooting tutakuwa mambo mbalimbali ya kufanya tukianzia kwenye jamii kwa maana tutakutana na wadau, wakazi wa Mkoa wa Pwani hasa Kibaha na Mlandizi ambako timu hii ipo.

“Tutazungumza kwa pamoja nini tufanye kuhakikisha kwamba malengo ambayo uongozi Ruvu Shooting imejiwekea msimu huu kuyafikia yanafikiwa,”amesema Bwire.

Ameeleza kuwa kati ya malengo yao msimu wa 2021/22 ni kuchuku kombe la ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na wakikosa ni kuhakikisha wanapata nafasi ya kuwakilisha nchi katika michuano ya Kimataifa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,750FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles